Nafasi za Matunda
Ujenzi wa Moyo na Makusanyo ya Tamaa
Ujenzi wa moyo uko katika mambo manne:
Katika elimu, taqwa, kumtii Mungu, na kumdhukuru Mungu.
Uharibifu wa moyo unatokana na mambo manne:
Kutokana na ujinga, uasi, kudanganyika, na ughafilifu.
Na makusanyo ya tamaa ni tano: Nayo ni katika kauli ya Mungu Mtukufu: ﴿Hakika maisha ya dunia ni mchezo na burudani na pambo na kujifakharisha baina yenu na kushindana kwa wingi wa mali na watoto﴾.
Mola awasalie Bwana wetu Muhammad na Aali zake na Masahaba zake wote
Na Assalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh