Vito Vizuri vya Matunda
Je, Unataka Kuwa Huru Kutoka Motoni?
Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani zimshukie (Yeyote asemaye: Ee Mwenyezi Mungu, mimi ninakushuhudia na ninawashuhudia Malaika Wako na wachukuzi wa Arshi Yako, na ninawashuhudia waliomo katika mbingu na waliomo katika ardhi, kwamba Wewe Ndiye Mwenyezi Mungu, hapana mungu ila Wewe, Wewe pekee huna mshirika, na ninashuhudia kwamba Muhammad ni mja Wako na Mtume Wako. Yeyote atakayesema mara moja, Mwenyezi Mungu atamwacha huru theluthi yake kutoka Motoni, na yeyote atakayesema mara mbili, Mwenyezi Mungu atamwacha huru theluthi mbili yake kutoka Motoni, na yeyote atakayesema mara tatu, Mwenyezi Mungu atamwacha huru yeye mzima kutoka Motoni.) Amesahihisha Albani
Rehema za Mwenyezi Mungu zimshukie Bwana wetu Muhammad na Aali zake na Masahaba zake wote
Na Amani iwe juu yenu na Rehema za Mwenyezi Mungu na Baraka zake