Nafaisi Al-Thamarati
Yeye ndiye aliyewapelekea watu wasiojua kusoma na kuandika Mtume kutoka miongoni mwao
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: ﴿Yeye ndiye aliyewapelekea watu wasiojua kusoma na kuandika Mtume kutoka miongoni mwao, anawasomea Aya zake na anawatakasa na anawafunza Kitabu na Hikima, ingawa kabla ya hapo walikuwa katika upotofu ulio wazi﴾.
Amesema Imamu Twabari: Yaani: Hakika Mwenyezi Mungu amewafanyia hisani enyi watu wa Imani alipowapelekea Mtume kutoka katika nafsi zenu anawasomea Aya zake na anawatakasa katika yale mliyoyazua na katika yale mliyoyafanya, na anawafunza mema na mabaya ili mjue mema mkafanya na mabaya mkayaepuka, na anawajulisha radhi zake kwenu pale mtakapomtii ili muweze kuzidisha katika kumtii na mjiepushe na yale aliyoyachukia katika maasi yake, ili muweze kujinasua kutokana na adhabu yake, na mupate thawabu yake kutoka peponi mwake, ﴿ingawa kabla ya hapo walikuwa katika upotofu ulio wazi﴾ yaani: katika upofu wa Kijahiliya hawajui jambo zuri, wala hawatubu kutokana na jambo baya, viziwi kutokana na haki, vipofu kutokana na uongofu.
Rehema za Mwenyezi Mungu zimfikie Bwana wetu Muhammad na Aali zake na Masahaba zake wote
Na Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh