Zawadi Bora
Kwa Maulamaa wa Kiislamu, Wenye Ushawishi, Wenye Uwezo na Waislamu Wote
Enyi maulamaa wa Kiislamu, wenye ushawishi, wenye uwezo na Waislamu wote: Yatosheni kunyamaza mbele ya umwagaji damu, uvunjaji heshima, unyakuzi wa vitu vitakatifu, bali na kuondolewa Uislamu kutoka katika uhalisia wa maisha.
Yatosheni kufanya mchezo katika kutekeleza faradhi ya kuwahisabu watawala na kubainisha haki mbele ya sultani dhalimu, ambayo Mwenyezi Mungu amewafaradhishia, vipi kwa msaliti kibaraka, anayehukumu kwa yasiyo yaliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu.
Hamjabakiwa na fursa ya kuchagua baina ya kukaa na baina ya kufanya kazi kwa ajili ya kuangusha mifumo mibovu na watu wajinga na kusimamisha Khilafah Rashidah na kumsimika Khalifa mwadilifu!
Hakika haisimami Dini wala hazihifadhiwi heshima wala hausimami uadilifu ila kwa kusimamisha Khilafah na kumsimika Khalifa kwa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani zimshukie amesema: "Na atakayekufa na hali shingoni mwake hamna bay'ah amekufa kifo cha kijahiliya".
Kwa kumtegemea kikamilifu Mwenyezi Mungu, na kwa imani na itikadi ya ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na bishara ya Mtume wake صلى الله عليه وسلم simameni pamoja na Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kufanya kazi ya kurejesha maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah Rashidah ya pili juu ya njia ya Utume, na kumpa bay'ah Alimu Mkuu Atā bin Khalīl Abu Rashtah Amir wa Hizb ut Tahrir kuwa Khalifa juu ya kufanya kazi kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, mnajikinga naye na mnapigana nyuma yake, kwa kufuata kauli yake صلى الله عليه وسلم: "Hakika Imamu ni ngao mnapigana nyuma yake na mnajikinga naye" Alitoa Bukhari kutoka kwa Abu Huraira.
Tunawaomba kwa yale yanayowahuisha duniani na Akhera na yanawadhaminia utukufu katika pande mbili. Je, tumefikisha, basi itikieni, Je, tumefikisha, Ewe Mwenyezi Mungu shuhudia.
{Enyi mlio amini! Itikieni wito wa Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuwaiteni kwenye litakalo kuhuisha. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu huingilia baina ya mtu na moyo wake, na kwamba kwake Yeye mtakusanywa} (Al-Anfal: 24)
Na umshukie rehema Bwana wetu Muhammad na Aali zake na Masahaba zake wote.
Na Amani ya Mwenyezi Mungu na rehema zake na baraka zake ziwe juu yenu.