Thamanai Bora za Matunda
Sio Ajabu
Amesema Ibn Al-Qayyim, Mwenyezi Mungu amrehemu
- Haishangazi mja anayedhalilika kwa Mwenyezi Mungu na kumwabudu, wala hachoki kumtumikia pamoja na uhitaji wake na ufakiri wake kwake, bali ajabu ni ya Mwenye kumiliki anayejipendekeza kwa mja wake kwa aina za neema zake na kumfanyia ukarimu kwa aina za ihsani zake pamoja na utajiri wake kwake.
- Yatosha kwako kuwa na utukufu kwamba wewe ni mja wake, na yakutosha fahari kwamba Yeye ni Mola wako.
Mfano wa kuzaliwa kwa utiifu, kukua kwake na kuongezeka kwake
Mfano wa kuzaliwa kwa utiifu, kukua kwake na kuongezeka kwake, ni kama mbegu uliyopanda, ikawa mti, kisha ikazaa matunda, ukayala matunda yake, na ukapanda mbegu zake, kila kilichozaa kutoka humo, ukavuna matunda yake, na ukapanda mbegu zake. Na hivyo ndivyo maasi yanavyoendana. Basi atafakari mwenye akili mfano huu. Kwa hakika miongoni mwa thawabu za jema ni jema linalofuata baada yake, na miongoni mwa adhabu za uovu ni uovu unaofuata baada yake.
Rehema za Mwenyezi Mungu zimshukie Bwana wetu Muhammad na Aali zake na Masahaba zake wote.
Na Amani iwe juu yenu na Rehema za Mwenyezi Mungu na Baraka zake