Nafasi za Matunda
Mwenye kutengeneza siri yake, Mwenyezi Mungu hutengeneza dhahiri yake
Amesema Sufyan bin Uyainah: Watu wema walikuwa wakiandikiana baadhi yao kwa baadhi maneno haya: Mwenye kutengeneza siri yake, Mwenyezi Mungu hutengeneza dhahiri yake, na mwenye kutengeneza baina yake na Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu hutengeneza baina yake na watu, na mwenye kufanya kwa ajili ya Akhera yake, Mwenyezi Mungu humtosheleza mambo ya dunia yake.
Rehema za Mwenyezi Mungu zimshukie Bwana wetu Muhammad na Aali zake na Masahaba zake wote
Na Amani iwe juu yenu na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake