Hazina za Matunda
Kutoka kwa aliyekusanya sifa sita
Amesema Ali bin Abi Talib, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, "Yeyote yule atakayekusanya sifa sita, basi hataacha haja ya pepo wala njia ya kukimbilia moto":
Ya kwanza ni yule anayemjua Mwenyezi Mungu kisha akamtii.
Na akamjua shetani kisha akamuasi.
Na akaijua haki kisha akaifuata.
Na akajua batili kisha akaiogopa.
Na akaijua dunia kisha akaitupilia mbali.
Na akaijua akhera kisha akaitafuta.
Na rehema za Mwenyezi Mungu zimshukie Bwana wetu Muhammad, na ahli zake na masahaba zake wote.
Na Assalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh.