Nafasi za Matunda
Mfano wa Kuzaliwa, Kukua na Kuongezeka kwa Utiifu
Mfano wa Kuzaliwa, Kukua na Kuongezeka kwa Utiifu
Mfano wa kuzaliwa, kukua na kuongezeka kwa utiifu, ni kama kokwa uliloipanda, ikawa mti, kisha ikazaa matunda, ukayala matunda yake, na ukapanda kokwa zake, kila ilipozaa kitu, uliyakusanya matunda yake, na ukapanda kokwa zake.
Na ndivyo ufuatiliaji wa maasi ulivyo, basi mwenye akili na atafakari mfano huu. Kwani thawabu ya jema ni jema baada yake, na adhabu ya baya ni baya baada yake.
Na rehema za Mwenyezi Mungu zimfikie Bwana wetu Muhammad na Aali zake na Masahaba zake wote
Na Amani iwe juu yenu pamoja na Rehema za Mwenyezi Mungu na Baraka zake