Zawadi Bora
WALAHA HATAMJAALIA ALLAH KAFIRI JUU YA MUUMINI NJIA
Hakika kusimamisha Khilafa juu ya njia ya Utume kama alivyotoa bishara kwayo Mtume wa Mwenyezi Mungu صلى الله عليه وسلم, kunahitaji kwanza kuwa mamlaka ya Umma ni ya asili; na ili mamlaka ya Umma iwe ya asili ni lazima ifanye kazi kwa uwezo wake wa asili, na juhudi zake za asili, ikitumia uwezekano wake wa asili, ikimtegemea Mwenyezi Mungu pekee Subhaanahu, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (NA JUU YA ALLAH NA WATEGEMEE WAUMINI); ili iweze kuondokana na ushawishi wa kafiri (Amerika, Urusi, Uingereza, Ufaransa na kila dola yenye tamaa na nchi za Waislamu), Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: (WALAHA HATAMJAALIA ALLAH KAFIRI JUU YA MUUMINI NJIA) Basi pindi mamlaka ya Umma itakapo kuwa ya asili itakuwa na uwezo wa kuamua hatma yake na kutekeleza matakwa yake na kutekeleza kitabu cha Mola wake na kusimamisha Khilafa yake.
{ENYI MLIO AMINI! MUITIKIENI ALLAH NA MTUME ANAPOKUITENI KWENYE YALE YANAYOKUHUSHENI, NA MJUE YA KWAMBA ALLAH HINGILIA BAINA YA MTU NA MOYO WAKE, NA YA KWAMBA KWAKE YEYE MTAFUSHWA * NA ILINDENI FITNA ISIWAFIKIE PEKEE WALE WALIO DHULUMU MIONGONI MWENU, NA MJUE YA KWAMBA ALLAH NI MKALI WA ADHABU}
Na Rehema za Allah zimfikie Bwana wetu Muhammad na Aali zake na Masahaba zake wote
Na Amani iwe juu yenu na Rehema za Allah na Baraka zake