Vito Vya Matunda - ENYI WATU WETU, ITIKIENI MWENYE KUITIA KWA ALLAH
Vito Vya Matunda - ENYI WATU WETU, ITIKIENI MWENYE KUITIA KWA ALLAH

Enyi Waislamu

0:00 0:00
Speed:
October 29, 2025

Vito Vya Matunda - ENYI WATU WETU, ITIKIENI MWENYE KUITIA KWA ALLAH

Vito Vya Matunda

ENYI WATU WETU, ITIKIENI MWENYE KUITIA KWA ALLAH

Enyi Waislamu 

Hakika mmekwishajaribu kwa miongo kadhaa uongo na hila za mifumo yenu, ambayo ufisadi wake umewafika watu wote na kuwa gumzo la watoto na wakubwa, je! haijawadia kwenu kusimama na mifumo hii msimamo ambao unamridhisha Mola wenu na kuhifadhi dini yenu, na utume ujumbe wa wazi kwa watawala kwamba ikiwa wao wanaendelea katika ghadhabu za Mwenyezi Mungu ili wapate radhi za Magharibi makafiri, basi waende peke yao, kwa sababu hamtomkasirisha Mwenyezi Mungu kwa radhi ya yeyote katika viumbe vyake.


Hakika sisi katika Hizb ut-Tahrir tunakuiteni kwa yale ambayo ndani yake kuna utukufu wenu na ukombozi wenu na utiifu kwa Mola wenu, tunakuiteni kukataa mifumo yote ya kikafiri na kurudi kwenye sheria ya Mwenyezi Mungu kwa kufanya kazi na Hizb ut-Tahrir ili kusimamisha dola ya Khilafah kwa njia ya Utume ambayo ni ahadi ya Mola wenu na bishara ya Nabii wenu Mtukufu, na njama ya adui yenu, na njia yenu ya kupata utukufu wa dunia na thawabu za Akhera.


﴿ENYI WATU WETU, ITIKIENI MWENYE KUITIA KWA ALLAH NA MUAMINI YEYE ATAKUSAMEHEENI DHAMBI ZENU NA ATAKULINDENI NA ADHABU IUMIZAYO * NA YULE ASIYEMUITIKIA MWENYE KUITIA KWA ALLAH BASI HAWEZI KUMSHINDA ALLAH KATIKA ARDHI WALA HAWEZI KUWA NA WALINZI BADALA YAKE HAO WAMO KATIKA UPUZI ULIO WAZI﴾ 

Rehema za Mwenyezi Mungu zimshukie Bwana wetu Muhammad na Aali zake na Masahaba zake wote

Na Amani iwe juu yenu na Rehema za Mwenyezi Mungu na Baraka zake

More from null

Thamani za Matunda - Ni haki kwa yule anayejua kwamba mauti ndio mahali pake pa kuelekea

Thmani za Matunda

Ni haki kwa yule anayejua kwamba mauti ndio mahali pake pa kuelekea

Alisema Al-Hasan Al-Basri, Mwenyezi Mungu amrehemu: Ni haki kwa yule anayejua kwamba mauti ndio mahali pake pa kuelekea, na Kiyama ndio ahadi yake, na kusimama mbele ya Mwenye Nguvu, ndio mahali pake pa kushuhudia, huzuni yake iwe ndefu duniani, na hamu yake iwe katika matendo mema. 

Adabu za Al-Hasan Al-Basri, kujiepusha kwake na dunia na mawaidha yake

Na Abu al-Faraj Ibn al-Jawzi

Mwenyezi Mungu amfikishie rehema Bwana wetu Muhammad na ahli zake na masahaba zake wote

Na Amani iwe juu yenu na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake

Zawadi Bora - Kukamilisha Kazi Mara Moja

Zawadi Bora

Kukamilisha Kazi Mara Moja

Miongoni mwa mambo yenye manufaa ni kukamilisha kazi mara moja, na kuwa na muda wa ziada katika siku zijazo kwa sababu kazi zisipokamilishwa, mabaki ya kazi zilizopita yatakusanyika, na kazi za baadaye zitaongezeka, na uzito wake utaongezeka, lakini ukikamilisha kila kitu kwa wakati wake, utafanya mambo yajayo kwa nguvu ya mawazo na nguvu ya kazi. 

Njia za Kufurahia Maisha kwa Furaha

Na Ibn Saadi

Mwenyezi Mungu amfikishie rehema Bwana wetu Muhammad, ahli zake na masahaba zake wote

Na Amani iwe juu yenu na Rehema za Mwenyezi Mungu na Baraka zake