Machapisho ya Hivi Karibuni

Makala Iliyoangaziwa

null

null

Soma zaidi
Msururu wa "Utawala na Uimamu katika Fikra ya Kiislamu" na Mwandishi na Mwanafikra Thair Salama - Abu Malik - Sehemu ya 73

Msururu wa "Utawala na Uimamu katika Fikra ya Kiislamu" na Mwandishi na Mwanafikra Thair Salama - Abu Malik - Sehemu ya 73

Ama yale yanayohusiana na utengano baina ya (Mamlaka Tendaji) na (Mamlaka ya Kimahakama), Uislamu haufanyi mamlaka ya kimahakama kuwa imetengana na mamlaka tendaji. Mara nyingi kadhi alikuwa akikusanya katika mamlaka yake katika hukumu majukumu mengine tendaji, kama vile uongozi wa jeshi kwa mfano. Hata hivyo, mimi naona kwamba kutenganisha mamlaka tendaji na mamlaka ya kimahakama ni miongoni mwa mambo ambayo uamuzi wake umeachwa kwa mwenye mamlaka. Akiona kwamba kutenganisha baina yao ndiyo njia ya kuhakikisha usalama wa hukumu, basi atenganishe. Na akiona kwamba kuwakusanya katika chombo kimoja kunaharakisha utekelezaji wa hukumu, basi awakusanye.

Jarida la Al-Raya: Jibu la Swali Kuhusu Mkakati wa Marekani na Suluhisho la Mataifa Mawili

Jarida la Al-Raya: Jibu la Swali Kuhusu Mkakati wa Marekani na Suluhisho la Mataifa Mawili

Tunajua kwamba mkakati wa Marekani kuhusu kuimarisha taasisi ya Kiyahudi katika moyo wa nchi za Kiislamu mara nyingi umekuwa ukiegemea suluhisho la mataifa mawili... Lakini katika enzi ya Trump, ulianza kupungua au angalau kunyamaziwa, jambo ambalo liliufanya uwe wa kutiliwa shaka... Kwa mfano, Trump alisema (Ninapotazama ramani ya Mashariki ya Kati, naiona Israeli kama doa dogo sana. Kwa kweli, nilisema kuna njia yoyote ya kupata maeneo? Ni madogo sana... Sky News, 2024/8/19) Je, hii inamaanisha kwamba mradi wa Marekani wa suluhisho la mataifa mawili umekufa na kumalizika au unabaki? Asante.

Jarida la Al-Raya: Kupenya kwa Wayahudi ndani ya Taasisi ya Kijeshi ya Misri

Jarida la Al-Raya: Kupenya kwa Wayahudi ndani ya Taasisi ya Kijeshi ya Misri

Tangu utawala wa Misri uliposaini mkataba wa Camp David mwaka 1979, taasisi ya kijeshi ya Misri iliingia katika mkondo wa utegemezi na kupenya, jambo ambalo liliifanya iwe mbali na itikadi yake ya asili iliyoanzishwa kwa misingi ya kulinda taifa na kutetea mipaka yake dhidi ya maadui zake wa kweli, na miongoni mwao ni Wayahudi waliokwapua Palestina. Taasisi hii imebadilika polepole kuwa chombo kilichofungwa, kinachotii masharti ya adui, na hata kushiriki katika kumlinda na kumwezesha, kupitia makubaliano ya kijeshi, kiusalama, kiuchumi na ushauri, ambayo yameunda mfumo kamili wa ushawishi wa Wayahudi ndani ya jeshi na serikali.

118 / 10603