Gazeti la Ar-Raya: Tofauti Kubwa Kati ya Taarifa ya Istanbul na Fatwa Zilizotangulia!
Wanazuoni walikusanyika katika ukarimu wa Erdoğan mwishoni mwa kongamano lao walilo liita "Gaza ni jukumu la Kiislamu na kibinadamu" lililo fanyika Istanbul kwa muda wa siku sita, walitoa taarifa ya mwisho ambayo waliifungua kwa aya za maandalizi na jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu mpaka yule anaye soma alidhani kwamba yale yatakayo kuja baada ya hapo kutoka kwa vifungu na maamuzi hayatakuwa ila ni taarifa ya kivitendo ya jinsi ya kujihusisha mara moja katika jihadi ambayo haimuokoi Gaza tu bali inakomboa Palestina na Msikiti wa Al-Aqsa.