Marekani Yaanzisha Kituo Kipya cha Kijeshi huko Damascus Kujumuishwa na Vituo Vyake vya Uhalifu katika Ukanda
Shirika la habari la Reuters liliripoti, mnamo Novemba 6, 2025, likinukuu vyanzo sita vyenye taarifa, wakiwemo maafisa wa Magharibi na afisa wa ulinzi wa Syria, kwamba Marekani inajiandaa kuanzisha uwepo wa kijeshi katika kambi ya anga iliyopo katika mji mkuu wa Syria, Damascus, au karibu nayo, kama sehemu ya mpango mpya unaosimamiwa na utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump. Kulingana na vyanzo, lengo la uwepo huu wa kijeshi ni kusaidia kufuatilia na kuwezesha utekelezaji wa makubaliano ya kina ya usalama ambayo kwa sasa yanajadiliwa kati ya Syria na chombo cha Kiyahudi kwa upatanishi wa Marekani.