Lengo la Trump katika Kukutana na Putin ni Lipi?
Katika mkutano na wanahabari tarehe 2025/8/11, Trump alisema: (Itakuwa mkutano wa kwanza kwa kiasi kikubwa... Nitamwambia Putin kabla ya mkutano, lazima uishe vita hii, lazima uisimamishe, na hatanichezea tena baada ya hapa), na aliongeza akionyesha kwamba anaweza kujiondoa kutoka kwa diplomasia kuhusu Ukraine (na ninaweza kutoka baada ya hapo na kutakia heri na suala linaisha), (na kwamba haliwezi kutatuliwa). Alisema atajua katika dakika za kwanza za mkutano ikiwa kuna uwezekano wa kufikia amani na Urusi, na pia alielezea kutoridhika kwake na matamshi ya Zelensky, ambaye alisisitiza kwamba atahitaji idhini ya kikatiba kuhusu masuala ya kikanda, na akatangaza kwamba mkutano utakuwa tarehe 2025/8/15 katika jimbo la Alaska la Marekani.