Machapisho ya Hivi Karibuni

Makala Iliyoangaziwa

null

null

Soma zaidi
Njia ya kujiondolea hatia ya kuwaangusha watu wa Palestina ni kufanya kazi usiku na mchana ili kusimamisha Khilafa Rashidah, na kuhamasisha vikosi vya jeshi

Njia ya kujiondolea hatia ya kuwaangusha watu wa Palestina ni kufanya kazi usiku na mchana ili kusimamisha Khilafa Rashidah, na kuhamasisha vikosi vya jeshi

Kwa sababu ya kutochukua hatua kwa majeshi ya Waislamu kumnusuru Gaza, baba mwingine aliyedhulumiwa, Abu Omar, ameuawa akiwa anatafuta riziki kwa ajili ya watoto wake. Alipokuwa akisubiri msaada, risasi ya mpiga risasi Myahudi mwoga ilipenya kichwani mwake. Ama rafiki aliyerudisha mwili wake, alikuwa na njaa kwa siku tano, na alirudi kutoka kwenye mlango wa shahada, na huenda akafa shahidi hivi karibuni. Hili si tukio moja tu, bali makumi ya matukio kama haya kila siku yanashuhudiwa na umma wa watu bilioni mbili!

Vyombo vya Ukandamizaji vya Mfumo wa Jordan Vinamkamata Sheikh Saeed Radwan kutoka Hizb ut-Tahrir

Vyombo vya Ukandamizaji vya Mfumo wa Jordan Vinamkamata Sheikh Saeed Radwan kutoka Hizb ut-Tahrir

Wakati watu wa Jordan wanapokwenda kutoka kaskazini hadi kusini na aina zao zote za hasira na mshikamano na Gaza, ambayo inaangamizwa na watu wake wanaanguka kutokana na njaa ya kikatili iliyowekwa juu yao na chombo cha Kiyahudi cha uhalifu na kwa ushirikiano wa kudhalilisha kutoka kwa mfumo wa Jordan, badala yake vyombo vyake vya ukandamizaji vinasimama dhidi ya hasira hizi kwa ukandamizaji na kukamatwa kikatili kwa wana wa umma na watu wake waaminifu...

Enyi Maulamaa wa Al-Azhar: Ikiwa hamtasema neno la haki leo... basi lini?!

Enyi Maulamaa wa Al-Azhar: Ikiwa hamtasema neno la haki leo... basi lini?!

Wakati ambapo vipindi vya mauaji ya kikatili ya Wayahudi huko Gaza vinaongezeka, na chakula, dawa na maji yananyimwa watoto, wanawake na wanaume, Al-Azhar ilitoa taarifa ikilaani "uhalifu wa njaa" unaofanywa na taasisi ya Wayahudi wahalifu. Taarifa hiyo ilifutwa baadaye! Je, inaruhusiwa kilio cha kumlalamikia dhalimu kufutwa?! Na je, sauti ya maulamaa itanyamaza mbele ya mauaji?! Taarifa hiyo ilikuja ikiwa imebeba misemo ya kibinadamu, ambayo inachochea (watu wenye dhamiri hai, jumuiya ya kimataifa, na nguvu zenye ushawishi), na inatoa wito wa kufunguliwa kwa vivuko na utoaji wa misaada.

Kilio kutoka Gaza Hashem... "Nyinyi ni maadui zetu Siku ya Kiyama"

Kilio kutoka Gaza Hashem... "Nyinyi ni maadui zetu Siku ya Kiyama"

Abu Ubaida alitoka, si kama alivyotoka jana akiwa mpiganaji, bali alitoka wakati huu akiwa amejeruhiwa, mwili mwembamba, mwenye maumivu makali, akiwa na sauti ya kukata tamaa ambayo haikutokana na udhaifu katika kupambana na adui, wala ukosefu wa silaha, bali kutokana na kisu moyoni kinachoitwa "usaliti wa umma", alisema kama radi: "Nyinyi ni maadui zetu Siku ya Kiyama"! Ndiyo, alisema amechelewa "Nyinyi ni maadui zetu Siku ya Kiyama", lakini sasa imefika na imeenea duniani, na kabla yake ilisemwa mara nyingi na vijana wa Gaza, wanaume wake na watoto wake ambao hawakuonyeshwa na vyombo vya habari vya nchi, lakini walionekana kwenye mitandao ya kijamii wakiomba msaada kwa umma, majeshi yake na wanazuoni wake, lakini hakuna anayejibu, miito yao haikugusa ujasiri wa Al-Mu'tasim kwa sababu hatuna dola, hatuna khalifa, hatuna ukhalifa!

204 / 10603