Kuhamasisha Watu Wenye Nia ya Kufanya Wajibu Wao
Amesema Mwenyezi Mungu: ﴿NA TUMEKUTEREMSHIA KITABU KIELEZO CHA KILA KITU﴾, basi ubainifu huu wa Kiungu unasisitiza kuwa Uislamu si mawaidha tu ya kiroho, bali ni mfumo kamili wa maisha, umekuja na itikadi thabiti inayoshawishi akili na kujaza moyo utulivu, na kwa hukumu zinazoongoza maisha ya mwanadamu katika mambo yake yote: katika utawala, uchumi, jamii, siasa, elimu na uhusiano wa kimataifa... Hakika hii ni dini ya haki, kwa sababu inatoka kwa Mwenyezi Mungu, na imejengwa juu ya msingi imara, nayo ni itikadi ya Kiislamu ambayo mfumo hutokana nayo, hivyo basi uhusiano wa mwanadamu nayo unakuwa ni wa kiakili kwa ushawishi, siyo kwa kufuata wala hisia, basi inakubaliana na fitra njema na inazungumza na akili, na kwa hivyo anayemwamini kwa imani timamu hawezi ila kuubeba na kuulingania na kupigania kuudhihirisha na kuutekeleza,