Habari na Maoni

Kuangamia kwa Taasisi ya Kiyahudi Siyo Udanganyifu

Kuangamia kwa Taasisi ya Kiyahudi Siyo Udanganyifu

Gazeti la Maariv lilisema, Jumatatu: "Kwa mara ya kwanza, jeshi linakiri kwamba kupungua kwa nguvu zake ni kubwa, lakini ni ndogo ikilinganishwa na wigo wa majukumu yake, na linakadiria kuwa linakosa takriban askari 7,500." Gazeti hilo liliongeza: "Jeshi kwa sasa linakabiliwa na upungufu wa maafisa 300 katika nafasi za viongozi wa vikosi katika mfumo wa mapigano wa vikosi vya ardhini." Jeshi, kulingana na Maariv, lilikiri kwamba "ni vigumu kuwashawishi askari wazuri kujiunga na kozi ya maafisa, na ili kukabiliana na pengo hilo, wasimamizi wakongwe wameteuliwa kuwa viongozi wa vikosi kwa niaba." (Raai Al-Youm)

Trump Anadai Hamas Haitaki Makubaliano ya Kusitisha Vita na Hamas Yakana

Trump Anadai Hamas Haitaki Makubaliano ya Kusitisha Vita na Hamas Yakana

Rais wa Marekani Donald Trump amedai kwamba harakati ya Hamas haitaki kweli kufikia makubaliano yanayoongoza kwenye kusitishwa kwa vita vya Wayahudi dhidi ya Gaza, huku Waziri Mkuu wa Wayahudi Netanyahu akisisitiza kwamba shirika lake linachunguza chaguzi za kuwarejesha mateka. Katika matamshi yake siku ya Ijumaa kutoka bustani ya Ikulu ya White House, Trump alisema kwamba kutakuwa na mapigano na kuangamizwa kwa Hamas, kwani "haitaki kufikia makubaliano, na nadhani inataka kufa." Aliongeza kuwa utawala wake umejiondoa kwenye mazungumzo ya Gaza, na kwamba hili ni jambo la kusikitisha, akishutumu Hamas kwamba haitaki kufikia makubaliano,

Mfumo wa Jordan Unacheza Juu ya Fuvu za Watu wa Gaza kwa Kufadhili Tamasha la Jerash!

Mfumo wa Jordan Unacheza Juu ya Fuvu za Watu wa Gaza kwa Kufadhili Tamasha la Jerash!

Tovuti ya Al Mamlaka ilichapisha siku ya Jumanne, Julai 22, 2025, matamshi ya Waziri Mkuu wa Jordan, Jaafar Hassan, wakati wa kikao cha Baraza la Mawaziri katika Mkoa wa Jerash kuhusu ufunguzi wa Tamasha la Jerash, ambapo alisema: Tamasha la Jerash ni muhimu kwa uchumi wa mkoa na sekta ya utalii nchini Jordan, ambayo serikali inafanya kazi kwa uwezo wake wote na njia zake kuunga mkono na kukuza licha ya mazingira ya kikanda yanayoizunguka, na akaongeza: Shughuli za Tamasha la Jerash zitaanza Jumatano, akitumaini kuwa tamasha la mwaka huu litakuwa la kipekee zaidi na uwepo kuliko miaka yote iliyopita, kwani ni moja ya matamasha maarufu ya Kiarabu.

Na Mwenyezi Mungu Ndiye Mwenye Utukufu Wote

Na Mwenyezi Mungu Ndiye Mwenye Utukufu Wote

Siku ya Alhamisi, Baraza la Seneti lilipitisha kwa kauli moja azimio la kulaani tukio la kuuawa kwa wanandoa wawili mchana kweupe kwa amri ya baraza la jirga kwa jina la kile kinachoitwa "uhalifu wa heshima" huko Balochistan. Azimio hilo lilisema kuwa uhalifu huu wa kinyama hauwezi wala haupaswi kufichwa chini ya kisingizio chochote cha kiutamaduni, kikabila au kimapokeo, kwa kisingizio cha kile kinachoitwa "wivu" au "heshima". Kwa hakika ni uhalifu ambao umeudhalilisha sana heshima ya taifa. Jaribio lolote la kuhalalisha uhalifu huu kwa msingi wa "desturi au heshima" limekataliwa kabisa, kama ilivyo kwa mchakato mzima wa kulaumu mhasiriwa.

7 / 1315