Msururu wa "Ukhalifa na Uimamu katika Fikra ya Kiislamu"
Kwa Mwandishi na Mwanafikra Thaer Salama – Abu Malik
Sehemu ya Arobaini na Nane: Falsafa ya Uislamu kuhusu Ukhalifa – J1
Ukhalifa ni kusimama kitu mahali pa kitu, na hukumu ni ya Mwenyezi Mungu, na amewajaalia viumbe kwa ujumla kwa kauli yake ﷺ: «Hakika dunia ni tamu na ya kijani kibichi, na Mwenyezi Mungu anakufanyeni makhalifa ndani yake, ili aone mnavyotenda» Imepokewa na Muslim kutoka kwa Abu Saeed Al-Khudri, kuthibitisha kauli yake Mwenyezi Mungu ﴿Kisha tukakufanyeni makhalifa katika ardhi baada yao ili tuone mnavyotenda﴾ [Yunus: 14]1, yaani mtekeleze hukumu za Mwenyezi Mungu, na manhaj ya Mwenyezi Mungu baina yenu na juu ya nafsi zenu katika kila jambo, na ukhalifa kwa khasa katika hukumu, kutoka kwa mtawala anahukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, kwani manhaj hii ndio inayotofautisha baina ya anayefanywa khalifa katika ardhi awe ni mharibifu ndani yake, mtoaji damu, au awe ni khalifa anaye kingwa na manhaj hiyo kutokana na kosa hilo, na ili itawale manhaj lazima itawale kupitia dola, siyo tu kwamba wafuate watu katika jamii ambayo inatawaliwa na manhaj isiyo hiyo!
Amesema Mwenyezi Mungu: ﴿Hakika Mimi nitaweka katika ardhi khalifa﴾ Alisema Al-Qurtubi Mwenyezi Mungu amrehemu: Aya hii ni asili katika kuteua imamu na khalifa anasikilizwa na kutiiwa; ili kusanyika neno naye, na zitekelezwe kwake hukumu za khalifa. Na hakuna khilafu katika wajibu wa hilo baina ya umma wala baina ya maimamu ila aliyo simuliwa kutoka kwa Al-Asam kwani alikuwa kuhusu sheria ni kiziwi, mwisho, na hili ni katika usahihi wa elimu ya Imamu Al-Qurtubi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake!
Na hiyo ni kuwa Mwenyezi Mungu ameisimamisha mbingu na ardhi juu ya uadilifu, kama ilivyo katika hadithi Qudsiy kutoka kwa Abu Dhar Jundub bin Junada, Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kutoka kwa Nabii ﷺ katika anayo simulia kutoka kwa Mwenyezi Mungu Tabaraka wa Ta'ala ﷻ, Mola wa Ukuu, zimetakasika majina yake kwamba amesema: «Enyi waja wangu mimi nimeharamisha dhulma juu ya nafsi yangu na nimeifanya baina yenu ni haramu basi msidhulumiane», basi Mwenyezi Mungu ameharamisha dhulma juu ya nafsi yake, na ameiharamisha juu ya waja na akateremsha sheria, na manhaj ambayo inahakikisha kwamba hauingii uonevu katika ufalme wa mbingu na ardhi, akamfanya mwanadamu kuwa khalifa ili asimamishe mfumo ambao unasimamisha uadilifu, na unazuia uonevu, ﴿Hakika tuliwatuma Mitume wetu kwa hoja zilizo wazi, na tukateremsha pamoja nao Kitabu na Mizani, ili watu wasimame kwa uadilifu﴾ [Al-Hadid: 25], akajaalia mamlaka kwa umma inamuwakilisha hakimu anayewahukumu kwa sheria ya Mola wake, kama ilivyo thibiti kutokana na kuchimbua kutoka katika asili za mfumo wa utawala katika Uislamu, basi khalifa aliyetajwa ni waumini wanaofuata sheria ya Mwenyezi Mungu katika aliyo waamrisha kuyasimamisha katika maisha yao, wanaosimamisha manhaj yake ndani yao, kama tulivyo tanguliza, kwani kusimama manhaj katika watu binafsi hakuiamishi katika jamii, na isiposimama katika jamii haitatimia kuhukumu kwao kwake2, na wala hautatimia uadilifu, kwa hivyo imepelekea jambo kusimama manhaj katika watu binafsi na jamii na dola, na kwani hukumu nyingi kati ya hizi zinatumiwa kupitia dola, basi watu humpa bai'a juu yake khalifa anazisimamisha ndani yao, basi lilikuwa kujaaliwa khalifa hakimu pia ni maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu: ﴿Na pale Mola wako alipo waambia Malaika: Mimi nitaweka katika ardhi khalifa﴾, yaani ambaye kwake inatimia maana ya kutafutwa ukhalifa utimia unaopelekea makusudio kutokana na utafutaji huo, katika anayodokeza aya kama alivyochimbua Al-Qurtubi, kwa hivyo waliuliza Malaika Mola wa Ukuu Subhanahu wa Ta'ala: ﴿Wakasema: Utamuweka humo atakaye fanya ufisadi na kumwaga damu?﴾ khalifa? Akasema haki Ta'ala akijibu: ﴿Akasema: Hakika Mimi najua msiyo yajua﴾, na wala si katika maana kuwa khalifa ni sitiari kuhusu mwanadamu anafanya analo taka, lau ingelikuwa hivyo, ingelitimia maana ya kukataa kwao: ﴿Wakasema: Utamuweka humo atakaye fanya ufisadi na kumwaga damu?﴾, ama kwani amewajibu Mola wa Ukuu akisema: ﴿Hakika Mimi najua msiyo yajua﴾ basi ndani yake mna maana kwamba hakumfanya khalifa kwa ajili ya kumwaga damu, na kufanya ufisadi, na kutokana na hili tunawatoa katika utafutwaji anayefuata manhaj yoyote inapelekea kufanya ufisadi na kumwaga damu, na huu ni hali ya kila manhaj iliyosimama juu ya kutunga sheria watu, na matamanio yao, kuthibitisha kauli yake Mwenyezi Mungu: ﴿Na lau Haki ingelifuata matamanio yao, zingelifisidika mbingu na ardhi na vilivyomo﴾ [Al-Mu'minun: 71], ﴿Kisha tukakuweka juu ya sheria katika jambo basi ifuate wala usifuate matamanio ya wasiojua﴾ [Al-Jathiya: 18], basi isiyo sheria ya Mwenyezi Mungu ni kufuata matamanio ya watungao sheria, na inapelekea kufanya ufisadi katika ardhi, kwa hivyo khalifa anayeashiriwa ni ambaye anasimamisha manhaj ya Mwenyezi Mungu ambayo inahakikisha kuthibitisha haki na uadilifu kulingana na sheria ya Mwenyezi Mungu, kwa kutumia sheria yake huyu ndiye aliyemtafuta Mwenyezi Mungu Ta'ala: Waumini wanasimamisha sheria yake na wanamupa bai'a khalifa anaitumia ndani yao.
Na akasema Mola wa walimwengu Subhanahu wa Ta'ala: ﴿Ewe Daudi! Hakika tumekufanya khalifa katika ardhi, basi hukumu baina ya watu kwa haki, wala usifuate matamanio yakakupoteza njia ya Mwenyezi Mungu﴾ [Sad: 26], na hiyo inalingana na kuwa Mwenyezi Mungu ameteremsha vitabu vhukumu baina ya watu kwa haki, ﴿Watu walikuwa umma mmoja, kisha Mwenyezi Mungu akawapeleka Manabii, watoao bishara na waonyaji. Na akateremsha pamoja nao Kitabu kwa Haki ili kihukumu baina ya watu katika yale waliyo khitalifiana﴾ basi kumtafuta Daudi Amani iwe juu yake na kuhukumu kwake baina ya watu kwa haki ni kama kumtafuta Muhammad ﷺ na kuhukumu kwake baina ya watu kwa haki ﴿Na uhukumu baina yao kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao, na tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu﴾ [Al-Maidah: 49], na hii ndani yake mna khitabu kwa Mtume ﷺ na ni khitabu kwa umma wake, basi kutafuta ilikuwa kusimama kwa hukumu za Mwenyezi Mungu katika waja, na ndio asili katika kila sheria ya kimungu, na kila kitabu kilicho teremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu kimeteremshwa ili kihukumu, na walikuwa wana wa Israel wanatawaliwa na Manabii kwa vitabu hivyo na sheria za kimungu, kisha ikahamia sunna hii kwa Makhalifa baada ya Mtume ﷺ kama ilivyo katika hadithi ya Bukhari kutoka kwa Abu Hazim alisema: Nilikaa na Abu Huraira miaka mitano nikamsikia anasimulia kutoka kwa Nabii ﷺ alisema: «Walikuwa wana wa Israel wanatawaliwa na Manabii kila alipoangamia Nabii alifuatwa na Nabii, na hakika hakuna Nabii baada yangu na watakuwa Makhalifa watakuwa wengi, walisema unatatuamrisha nini? Alisema: timizeni bai'a ya wa kwanza kisha wa kwanza na wapeeni haki yao, kwani Mwenyezi Mungu atawauliza kuhusu walicho pewa kukichunga» [Imepokewa na Muslim na Bukhari na Ibn Hanbal na Ibn Majah], basi ametaja kwamba siasa ya umma itakuwa kwa Nabii ﷺ kisha kwa Makhalifa baada yake, na akaamrisha kuwatii na kutimiza bai'a yao, na kutoka kwa Abu Saeed Al-Khudri kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ kwamba alisema: «Akipewa bai'a Makhalifa wawili basi muuweni yule mwingine kati yao», akaamrisha umoja wa dola ya Ukhalifa na akamfanya anayetenganisha jamaa ya Waislamu ni halali ya damu, amesimulia Muslim katika kitabu cha Uimara: «Kutoka kwa Arfaja alisema nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ anasema anayekujieni na amri yenu ni jamaa juu ya mtu mmoja anataka kuigawanya fimbo yenu au kuifarikisha jamaa yenu basi muueni».
1- Na kauli yake Mwenyezi Mungu Ta'ala: ﴿Naye ndiye aliyekufanyeni makhalifa katika ardhi, na akawainua baadhi yenu juu ya wengine kwa daraja, ili akujaribuni katika aliyo kupeni. Hakika Mola wako ni Mwepesi wa kuadhibu, na hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu﴾ 165 Al-An'am, na kauli yake Mwenyezi Mungu Ta'ala: ﴿Yeye ndiye aliyekufanyeni makhalifa katika ardhi﴾ 39 Fatir.
2- Jiwe la msingi katika utambulisho wa jamii ni namna ambayo zinaendeshwa kwayo mahusiano, na kanuni ambazo zinadhibiti mahusiano haya, basi mahusiano ya riba ni matokeo ya kutumia mfumo wa kirasilimali mathalan, haiwezekani kubadilika katika jamii maadamu imebakia jamii ni ya kirasilimali, na wala hakuna athari ya kukataa mamilioni ya watu miongoni mwa Waislamu katika jamii za kimagharibi au hata nchi za Kiislamu ambazo unatawanyika ndani yake mfumo wa riba kuhusu riba katika kubadilisha mfumo wa kiuchumi wa kirasilimali ndani yake, bali wao bila shaka zitaingia pesa zao benki, na zitazitumia benki kwa namna ya kisheria katika anayoyaona benki, na zichanganyike pesa za Waislamu na riba na na biashara ya pombe, na vitega uchumi ambavyo zinavitega benki katika vilabu vya usiku, wametaka Waislamu katika magharibi au wamekataa, bali na juu ya hivyo, basi watakubali sheria za dola kutokana na bima ya lazima, na kanuni zilizoharamishwa katika Uislamu na mengineyo, basi muhula kwa hivyo katika mahusiano na kanuni siyo katika itikadi za watu binafsi.