
12/8/2025
Abu Wadaha News: Umoja wa Umma na Umoja wa Dola ni Miongoni mwa Masuala ya Waislamu wa Misri, Akihutubia Hizb ut Tahrir Wilaya ya Sudan, Port Sudan
Katika kampeni inayoendeshwa na Hizb ut Tahrir / Wilaya ya Sudan, ya kufeli njama ya Marekani ya kuitenganisha Darfur, chama kilifanya hotuba ya kisiasa jioni ya Jumatatu, 17 Safar 1447 Hijria, sawia na 11/08/2025 Miladia, mbele ya Hoteli ya Haramain katika Soko Kuu katika mji wa Port Sudan, chini ya anwani: (Umoja wa Umma na Umoja wa Dola ni Miongoni mwa Masuala ya Msingi).
Ndani yake, Ustadhi Muhammad Jami Abu Ayman alitoa ujumbe mzito kwa umati wa waliohudhuria, akieleza njama ambayo makafiri wakoloni wanaiunda kuivunja nchi za Waislamu kupitia mradi wa Bernard Lewis (Mipaka ya Damu), ambapo mzungumzaji alieleza kuwa njama ya Marekani inayofuata baada ya kujitenga kwa Sudan Kusini, ni kuitenganisha Darfur. Ambapo alikusanya idadi ya ushahidi unaoonyesha uharamu wa kuvunja nchi za Waislamu, na kutoruhusu yeyote kuanzisha dola tofauti na mwili wa Umma, ikiwa ni pamoja na hadithi ya Mtume Muhammad (rehema na amani zimshukie): (Na yeyote atakayempa imamu ahadi, akampa mkono wake na matunda ya moyo wake, basi amtii ikiwa anaweza, na ikiwa mwingine atakuja na kumpinga, basi kata shingo ya huyo mwingine). Na hadithi: (Pindi watakapopewa bay'a makhalifa wawili, basi muuweni yule wa mwisho kati yao), na alieleza kuwa Uislamu ulifanya umoja wa dola kuwa suala la msingi wakati ulipokataza wingi wa makhalifa, na akaamrisha kuuliwa kwa yule anayejaribu kuleta wingi katika ukhalifa, yaani, chombo cha dola, au kurudi nyuma kutokana na tendo lake. Na hadithi: (Atakayewajieni hali mko pamoja juu ya mtu mmoja anataka kuipasua fimbo yenu au kuwatenganisha kundi lenu, basi muuweni), ambayo ilifanya suala la umoja wa Umma, na umoja wa dola kuwa suala la msingi wakati ilipokataza kuutenganisha kundi, na ikaamrisha kuuliwa kwa yule anayejaribu kufanya hivyo au kurudi nyuma kutokana na tendo lake.
Kisha mzungumzaji aliwaomba Waislamu waamke kama mtu mmoja, na wachukue hatua ya uhai au mauti dhidi ya majaribio ya makafiri na wasaidizi wao kuichuna Darfur, na hii inahitaji kupinga mipango ya kafiri mkoloni na kufanya kazi na wafanyakazi wa kusimamisha dola ya Waislamu Khilafah ambayo ndiyo dhamana ya kweli ya kuhifadhi nchi za Waislamu, na kuziunganisha katika chombo kimoja.
Na mwingiliano ulikuwa mzuri ambapo kulikuwa na maswali kuhusu jinsi serikali inavyoshughulikia kampeni ya silaha iliyoenea nchini Sudan, na katika nchi nyingi za Waislamu, hivyo mzungumzaji alijibu kwamba kushughulika na waasi ni kwamba ni haramu kumpinga yule ambaye uimamu wake umethibitishwa kisheria, kwa sababu katika kumpinga kuna mgawanyiko wa fimbo ya Waislamu, umwagaji damu yao, na upotezaji wa mali zao, kwa kauli yake (rehema na amani zimshukie): «Atakayemtokea umma wangu hali wote wamekusanyika, basi muuweni awe yeyote yule», basi hawa wanaompinga imamu wa kisheria ni waasi wanaotakiwa kutubu, na kuondolewa shaka zao, na wakiendelea kusisitiza watapigwa vita… Na yote hayo ni kwa ajili ya kuhifadhi umoja wa dola na umoja wa Umma na kuzuia kuutenganisha…
Ofisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan
Chanzo: Abu Wadaha News
