Vita Vilivyosahaulika vya Sudan: Janga kwa Umma
"Hofu inayofichuka nchini Sudan haina mipaka"
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Volker Turk
(Imetafsiriwa)
Sudan inavuja damu, na ulimwengu haujali. Sasa, vita vikali kati ya Jeshi la Wanajeshi la Sudan linaloongozwa na Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, na Vikosi vya Msaada wa Haraka vinavyoongozwa na Mohamed Hamdan Dagalo (Hemedti), vinaingia mwaka wake wa tatu, vikiwa vimeitumbukiza nchi katika machafuko na kuachilia moja ya majanga mabaya zaidi ya kibinadamu katika enzi yetu. Hata hivyo, licha ya ukubwa wa uharibifu na mateso, vita vya Sudan vinapuuzwa, vinasahaulika, na kunyamazishwa kutokana na kutojali kwa kimataifa.
Mzozo huu wa madaraka umegharimu maisha ya takriban raia 150,000 tangu Aprili 2023 - ingawa mashirika ya misaada yanaamini idadi halisi ni kubwa zaidi. Hawa si askari kwenye medani za vita, bali ni wanawake, watoto na wazee, wanaouawa bila huruma katika nyumba zao, misikiti, masoko na makambi yao ya muda (BBC). Mauaji ya Al-Nuhud, ambapo zaidi ya raia 300 waliuawa - wakiwemo watoto 21 - na wapiganaji wa Kikosi cha Msaada wa Haraka, ni moja tu ya ukatili usiohesabika. Miji yote imechomwa moto na kusawazishwa na ardhi. Makaburi ya halaiki yamechimbwa kwa haraka. Familia nzima zimetoweka. Kinachotokea Sudan sio tu vita, lakini mauaji ya kimbari ya kimfumo.
Wanawake na wasichana, kama ilivyo kawaida katika vita, ni miongoni mwa waathirika walio katika hatari zaidi ya unyanyasaji. Pande zote mbili zimetumia unyanyasaji wa kingono kama chombo cha ugaidi na utawala. Wasichana wadogo hadi umri wa miaka 9 walitekwa nyara, walibakwa kwa wingi, na kisha walirudishwa nyumbani kwao wakiwa wameharibiwa kimwili, ikiwa walirudi kabisa. Waathirika wanazungumzia kuhusu ubakaji wa hadharani unaolenga kuwadhalilisha jamii, na unyanyasaji wa kingono wa halaiki katika kambi za wakimbizi.
Wafanyakazi wa matibabu wanaripoti kuwatibu manusura bila kupata msaada wa kisaikolojia au haki. Wengi wao hukaa kimya kwa hofu ya aibu au kulipizwa kisasi. (Shirika la Human Rights Watch, Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu)
Zaidi ya watu milioni 14 wameyakimbia makazi yao, na kufanya hili kuwa janga kubwa zaidi la uhamaji ulimwenguni. Zaidi ya nusu ya watu wa Sudan, ambao ni milioni 50, wanakabiliwa na hatari ya njaa. Kulingana na Mpango wa Chakula Duniani, njaa imekumba angalau maeneo 10, ikiwa ni pamoja na kambi ya Zamzam, ambayo inahifadhi wakimbizi 400,000. (Mpango wa Chakula Duniani).
Chakula na maji ni adimu. Si kwa sababu ya janga la asili, bali kimakusudi. Makundi yote mawili yametumia njaa kama silaha kwa kuzuia misaada ya kibinadamu, kunyakua vifaa, na kuzuia ufikiaji wa mahitaji muhimu. Njaa inatumiwa kuadhibu watu wote.
Katika kambi za wakimbizi, watoto wanakula majani, na mama hupitisha siku bila chakula ili kulisha watoto wao. Magonjwa yanayosababishwa na maji, malaria na kipindupindu yameenea kwa kasi. Mifumo ya afya imebomoka. UNICEF inaeleza hali hiyo kuwa ni janga la pande nyingi, ambalo linaangamiza kila kipengele cha maisha; afya, usafi wa mazingira, elimu, na usalama. (Shirika la Afya Duniani). Ripoti nyingi zimeibuka kuhusu mateso ya wafungwa wa kisiasa, utekaji nyara wa raia, na kuandikishwa kwa watoto kulazimishwa kupigana. Wafanyakazi wa kibinadamu pia wamelengwa, wakiuawa, kutekwa nyara, au kuzuiwa kuwafikia wanaohitaji. Hospitali zimeporwa na kugeuzwa kuwa medani za vita. Shule zimebombwa. Hakuna mahali salama palipoachwa. (Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu).
Hata hivyo, vyombo vya habari havigitaji jina la Sudan. Vita hivyo vinaelezwa kuwa havionekani, vimesahaulika, au vimefutwa kabisa kutoka kwenye vichwa vya habari. Tofauti na Ukraine au Gaza, hakuna ridhaa kutoka kwa watu mashuhuri, hakuna maandamano ya umati, na hakuna uharaka wa kisiasa.
Ukimya wa Sudan si bahati mbaya, utajiri wake wa dhahabu, mafuta, uranium na ardhi yenye rutuba unaifanya kuwa zawadi ya kijiografia. Nguvu kama vile UAE, Saudi Arabia, Misri, Marekani, Uingereza na Urusi, zote zina maslahi nchini Sudan. Nchi hiyo imekuwa ubao wa chess kwa maslahi ya kigeni.
Vita nchini Sudan si bahati mbaya ya kihistoria. Ni urithi wa ukoloni, mipaka ya kugawanya, na udikteta wa kidunia unaoungwa mkono na wahisani wa kigeni. Sudan, kama ilivyo kwa mataifa mengi yaliyoanzishwa katika nchi za Waislamu, ilikuwa chini ya udhibiti wa mamlaka za kikoloni. Imenyimwa uhuru wa kweli, uongozi wake umeharibiwa, na watu wake wamegeukana dhidi ya wao kwa wao.
Suluhu za kidemokrasia zinazokuzwa na nchi za Magharibi ni sehemu ya tatizo. Mifumo hii - iliyoundwa kutumikia maslahi ya wasomi - imeiangusha Sudan, kama ilivyoangusha Iraq, Libya na Afghanistan.
Kuna njia moja tu inayotoa suluhu ya kweli na ya kudumu kwa Sudan na umma wa Kiislamu kwa ujumla. Njia hiyo ni kuanzisha Khilafah kwa msingi wa Utume.
Khilafah itawaunganisha Waislamu bila kujali kabila zao, itakomesha ushawishi wa kigeni, itagawa rasilimali kwa haki, itasimamisha kanuni ya uwajibikaji, na itahakikisha heshima na usalama kwa wote. Historia inakumbuka jinsi utawala wa Khilafah katika enzi ya Omar bin Abdul Aziz ulivyoondoa umaskini Afrika Kaskazini hadi iliposhindikana kupata mtu anayestahili kupokea Zaka.
Mtume ﷺ alisema: «Mfano wa Waumini katika kupendana kwao, kuhurumiana kwao, na kuoneana kwao, ni mfano wa mwili mmoja, ikiwa kiungo kimoja kinauma, mwili wote unaitikia kwa kukesha na homa» Sahih Muslim. Umma wetu nchini Sudan uko katika dhiki, ulimwengu hauwezi kujali, lakini ni lazima tujali.
Sehemu ya wanawake katika Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir inawaomba Waislamu wote kutoa ufahamu, kukataa suluhu batili, na kutoa wito wa kuanzishwa kwa haraka kwa dola ya Khilafah kwa msingi wa Utume.
﴿Enyi mlio amini! Itikieni wito wa Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuwaiteni kwenye litakalo kuuhisha﴾
#Mgogoro_wa_Sudan #SudanCrisis
Imeandikwa kwa ajili ya redio ya Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
Yasmin Malik
Mjumbe wa Ofisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir
