2025-08-13
Jarida la Al-Raya: Diplomasia ya Bahari kati ya Ugiriki na Libya
Katika Kukabiliana na Mkataba wa Uturuki na Libya
Ugiriki imeitaka serikali ya Libya inayotambuliwa kimataifa (Serikali ya Umoja wa Kitaifa mjini Tripoli) kuanzisha mazungumzo ya pande mbili kuhusu uwekaji mipaka ya bahari na maeneo ya kipekee ya kiuchumi (EEZ) katika Bahari ya Mediterania. Hatua hii inalenga kurekebisha uhusiano ulioharibika tangu kusainiwa kwa mkataba wa bahari wa Libya na Uturuki wenye utata mwaka 2019. Pia kushughulikia pingamizi za Libya kuhusu zabuni ya uchimbaji wa hidrokaboni iliyoanzishwa na Ugiriki karibu na kisiwa cha Krete na kuimarisha ushirikiano wa pande mbili, hasa katika kupambana na uhamiaji haramu kutoka Libya kuelekea visiwa vya Ugiriki (kama vile Krete na Gavdos)
Msingi wa moja kwa moja wa mvutano unatokana na kusainiwa kwa mkataba wa uwekaji mipaka ya bahari kati ya Serikali ya Upatanisho wa Kitaifa ya Libya na Uturuki mnamo Novemba 2019. Mipaka ilichorwa katika mkataba huu kwa njia ambayo inapuuza kabisa uwepo wa kisiwa cha Krete cha Ugiriki (na visiwa vingine vya Ugiriki), ambapo ilizingatiwa kama mstari ulionyooka kati ya pwani ya Libya na pwani ya Uturuki. Mkataba huo pia unaonyesha mwendelezo wa maono ya kikanda ya Uturuki kama mrithi wa Ukhalifa wa Ottoman, ambapo Ankara inahalalisha mkataba huo na haki za kihistoria zilizorithiwa kutoka kwa mikataba ya Ottoman, kama vile Mkataba wa Lausanne wa 1923, ambao Uturuki inauona haulazimishi mipaka yake ya sasa ya bahari.
Mwelekeo huu unajidhihirisha katika kutoa msaada wa moja kwa moja wa kijeshi kwa serikali ya Tripoli na Uturuki tangu 2019, kwa kuzingatia uhusiano wa kihistoria na msingi wa zamani wa majini katika enzi ya Ottoman. Wakati Ugiriki inakataa pendekezo hili, ikisisitiza kuwa sheria ya kisasa ya kimataifa inabatilisha uhalali wa kihistoria. Athens imeomba Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya kuiwekea Uturuki vikwazo, ikizingatia mkataba huo kuwa "ukiukaji wa uhuru."
Majibu ya Kimataifa:
Mkataba huu ulizua hasira kali nchini Ugiriki, Cyprus na Misri, na uliiona kama ukiukaji mkubwa wa sheria ya kimataifa ya bahari (UNCLOS) ambayo inawapa visiwa haki kamili za bahari. Pia ilikabiliwa na kulaaniwa na wito wa kufutwa kutoka Umoja wa Ulaya na Marekani, kwa hofu ya kuongezeka kwa mvutano katika eneo muhimu kwa usafiri wa baharini na nishati. Usaidizi wa Ulaya kwa Ugiriki kama kizuizi dhidi ya upanuzi wa Urusi katika Mediterania kupitia washirika kama Jenerali Haftar mashariki mwa Libya. Hata hivyo, Umoja wa Ulaya unaonyesha mgawanyiko wa ndani kati ya kuunga mkono Ugiriki kisiasa na hamu ya kuhakikisha usambazaji wa nishati kutoka Libya kupitia Uturuki.
Ama Urusi, inaona katika ushindani huu fursa ya kuimarisha uwepo wake wa kijeshi na kuzuia miradi ya njia za gesi zinazoshindana kama vile EastMed, ambayo inaweza kudhoofisha usafirishaji wa gesi ya Urusi.
China pia kupitia uwekezaji wake katika miundombinu ya Libya, ikifaidika na ombwe la usalama ili kuimarisha mradi wa Ukanda na Njia.
Wakati msimamo wa Misri unabadilika kati ya kupinga mkataba wa Uturuki kwa sababu unapingana na mipaka yake ya bahari, na ukaribu wa hivi karibuni na Ankara, haswa baada ya uvumbuzi wa gesi katika eneo la pamoja la Shuruq.
Kutumia Mgawanyiko wa Libya kama Chombo cha Kimataifa:
Serikali ya Tripoli inayoungwa mkono na Uturuki inashikilia mkataba wa bahari na Ankara, wakati serikali ya mashariki inaungana na Urusi na Misri. Mgawanyiko huu unanyima Libya umoja wa maamuzi na kuifanya uwanja wa mzozo wa kimataifa, ambapo mikataba inafanywa na upande mmoja bila idhini ya upande mwingine. Jambo ambalo linafanya wito wa Ugiriki, licha ya asili yake ya kisheria, kugongana na kikwazo cha msingi: ukosefu wa mamlaka moja nchini Libya.
Sababu kuu ya mzozo huo iko katika uwepo wa utajiri mkubwa wa gesi chini ya sakafu ya Mediterania, ambayo inafanya eneo hilo kuwa ngumu zaidi, kwani Uturuki inataka kuhakikisha sehemu kupitia makubaliano na Libya, wakati Ugiriki inataka kuzuia upanuzi huu kupitia ushirikiano na Misri, Kitengo cha Kiyahudi na Cyprus. Ama faili ya uhamiaji, Athens imeitumia kama njia ya kushinikiza, kwani inaitumia kuhalalisha kuimarisha uwepo wake wa baharini na kijeshi kusini. Kwa upande mwingine, Uturuki inatishia kutumia kambi za kijeshi za Libya kama njia ya kushinikiza, wakati Ulaya inaamua kuweka vikwazo vya kisiasa na kiuchumi. Hivyo, faili za uchumi, uhuru na uhamiaji zinaingiliana katika vita vya ushawishi katika eneo hilo.
Mikakati ya Kukabiliana na Mediterania: Kati ya Uanamajeshi wa Uturuki na Shinikizo la Ulaya:
Uturuki inategemea mbinu mbili katika kukabiliana na mzozo wa baharini, kijeshi kwa kupeleka meli zake za kivita kulinda operesheni za uchimbaji, na inatumia kambi zake magharibi mwa Libya kama msingi wa Al-Watiya kulazimisha hali halisi, na kidiplomasia kwa kutishia kuahirisha idhini ya Bunge la Libya kwa mkataba huo ili kuishinikiza Ulaya, ikitumia faili nyeti kama vile uhamiaji na forodha.
Kinyume chake, Ugiriki inataka kugeuza mzozo huo kuwa vita vya pamoja vya Ulaya, kwa kuonyesha mkataba wa Uturuki na Libya kama tishio kwa usalama wa pamoja ili kuvutia msaada wa NATO na Umoja wa Ulaya, na kutumia mzozo wa uhamiaji kutoka Libya kwenda visiwa vyake kama vile kisiwa cha Krete kama kisingizio cha kuimarisha uwepo wake wa baharini na kijeshi.
Ama matukio yanayowezekana, yanaelekea kwenye njia tatu tofauti; ama kuongezeka kwa kijeshi ikiwa Bunge la Libya litathibitisha mkataba huo, ambayo inaweza kupelekea Ugiriki kujibu kwa msaada wa muungano wa NATO, au kugawanya ushawishi kupitia mazungumzo ya pande tatu (Uturuki, Ugiriki, Libya) kwa usuluhishi wa Umoja wa Mataifa, kuhakikisha hisa katika utajiri wa Mediterania, au kuendelea kwa mkwamo kutokana na mgawanyiko wa ndani wa Libya na kutokuwa na uwezo wa nguvu za kimataifa kulazimisha suluhisho la mwisho.
Kuanzia hapa, inaonekana kuwa tukio la Libya na Ugiriki sio tu mzozo wa mpaka, lakini ni mfano wa mzozo mpana wa kijiografia, ambapo nguvu kubwa zinaunda upya ushirikiano wao katika ombwe la mamlaka la Libya, kwa kutumia urithi wa historia na utajiri wa siku zijazo. Uturuki itakuwa na jukumu kuu katika kupinga jaribio lolote la kudhoofisha mkataba wa 2019 au kupunguza ushawishi wake nchini Libya na mashariki mwa Mediterania. Badala yake, inaweza kuishinikiza Libya au kutoa ahadi na vitisho ili kudumisha hali ilivyo.
Hitimisho, kucheza na sheria za kimataifa hakuna maana, kwani kutasababisha migogoro ya pembeni na mzozo juu ya maslahi finyu ya kitaifa, ambayo huimarisha mgawanyiko wa nchi za kanda ndani ya ulimwengu wa nguvu kubwa zinazotawala ulimwenguni, wakati Waislamu wanateseka katika kiwango cha kwanza na moto wa sheria hii ya kimataifa, ambayo chini yake ubinadamu umeishi vita viwili vya uharibifu vya ulimwengu, ambayo kihistoria imeimarisha utawala wa nguvu kubwa juu ya Waislamu, na sheria zake zinapingana na masharti ya Uislamu kwa ujumla, badala yake ilikuwa nyuma ya majanga yetu mengi katika nyakati za kisasa, kutoka kuanguka kwa Ukhalifa hadi kugawanyika kwa nchi za Waislamu hadi kupanda kwa Kitengo cha Kiyahudi moyoni mwa Umma wa Kiislamu, hadi kile kinachotokea sasa huko Gaza, Sudan na nchi zingine za Waislamu. Kukatisha uhusiano na mfumo huu dhalimu hakutakuwa isipokuwa kwa kuanzisha dola ya Ukhalifa ambayo itaanza upya maisha ya Kiislamu, kulazimisha hali mpya ya kimataifa, na kurejesha haki ya kisheria na ya kihistoria ya Umma kwa kila inchi ya bahari, ardhi na anga ambayo imewahi kuwa chini ya mamlaka ya Uislamu, na dola ya Ukhalifa itafanya kazi tangu kuanzishwa kwake kuimarisha desturi za kimataifa ambazo zinainua wanadamu, kutetea waliofinywa, na kukomesha ukoloni, unyakuzi wa utajiri, na udanganyifu kwa watu walio katika mazingira magumu ulimwenguni, ﴿NA WALE WALIO DHULUMU WATAJUA NI MAHALI GANI PA KUREJEA WATARUDI﴾.
Imeandikwa na: Profesa Yassin bin Yahya
Chanzo: Jarida la Al-Raya
