Miongoni mwa Vipengele Vya Kisaikolojia vya Kiislamu - Kipindi Cha Tatu
Miongoni mwa Vipengele Vya Kisaikolojia vya Kiislamu - Kipindi Cha Tatu

Alhamdulillah Mola Mlezi wa walimwengu, na sala na salamu zimwendee Imamu wa wacha Mungu, na Bwana wa Mitume, aliyetumwa kama rehema kwa walimwengu, Bwana wetu Muhammad na ahli zake na masahaba zake wote, na tujaalie kuwa pamoja nao, na utukusanye katika kundi lao kwa rehema yako, Ee Mrehemu zaidi wa wote wenye kurehemu.

0:00 0:00
Speed:
November 02, 2025

Miongoni mwa Vipengele Vya Kisaikolojia vya Kiislamu - Kipindi Cha Tatu

Miongoni mwa Vipengele Vya Kisaikolojia vya Kiislamu

Kipindi cha Tatu

Alhamdulillah Mola Mlezi wa walimwengu, na sala na salamu zimwendee Imamu wa wacha Mungu, na Bwana wa Mitume, aliyetumwa kama rehema kwa walimwengu, Bwana wetu Muhammad na ahli zake na masahaba zake wote, na tujaalie kuwa pamoja nao, na utukusanye katika kundi lao kwa rehema yako, Ee Mrehemu zaidi wa wote wenye kurehemu.

Enyi Waislamu: 

Wasikilizaji wapenzi, wasikilizaji wa redio ya afisi ya habari ya Hizb ut-Tahrir:

Assalamu alaikum warahmatullahi wabarakatuh, na baada ya hayo: Katika kipindi hichi tunaendelea na tafakuri zetu katika kitabu "Miongoni mwa Vipengele Vya Kisaikolojia vya Kiislamu". Na kwa ajili ya kutoa mifano hai ya tabia ya Kiislamu, huku tukizingatia akili ya Kiislamu, tunasema na kwa taufiki ya Allah: Tulisema katika kipindi kilichopita: "Akili ni jinsi akili inavyoendesha mambo, yaani, kutoa hukumu juu yake kulingana na kanuni ambayo inaamini na kutulia nayo". Hivyo ndivyo Muislamu anapaswa kuwa akisimama kwenye mipaka ya Mwenyezi Mungu, akipima mambo kwa kipimo cha Mwenyezi Mungu, na kuipima kwa mizani ya Mwenyezi Mungu, ambayo ni halali na haramu, akifuata aliyoamrisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kuacha aliyokataza Mwenyezi Mungu na Mtume wake, akifanya hivyo hata kama inapingana na matamanio yake na maslahi yake akitafuta radhi za Mwenyezi Mungu, na hali ya ulimi wake inasema yale aliyosema mshairi: 

Laiti unakuwa mtamu ilhali maisha ni machungu                Na laiti unaridhika ilhali viumbe wamekasirika

Na laiti yale yaliyo baina yangu na wewe yamejengeka              Na baina yangu na walimwengu yameharibika

Ikiwa mapenzi yatakuwa sahihi kutoka kwako, basi kila kitu ni rahisi                Na kila kilicho juu ya ardhi ni ardhi

Enyi Waislamu: 

Muumini mwenye akili ya Kiislamu «mnyenyekevu, laini, mwerevu, mwangalifu». Kama alivyotueleza mpenzi wetu Mtume Mustafa, sala na salamu za Mwenyezi Mungu zimshukie, kwani muumini anasifika kwa busara na akili, naye ni mwepesi wa kufahamu, kwa maana kwamba katika hali ngumu na za hatari anajitahidi kwa hekima, akijibu jibu la kumnyamazisha adui yake, ambalo linamuokoa na kumwondolea dhiki na aibu, na kumtoa katika mkwamo aliyomweka adui yake, na tutatoa mfano hai wa maisha ya Mtume, swallallahu alayhi wasallam: Katika wasifu wa Ibn Hisham, Ibn Ishaq alisema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu, swallallahu alayhi wasallam, na Abu Bakr, Radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie, walipanda mpaka wakasimama juu ya mzee mmoja kutoka kwa Waarabu, wakamuuliza kuhusu Maquraishi na kuhusu Muhammad na masahaba zake na yale aliyoyasikia kuhusu wao, yule mzee akasema: Siwambii mpaka mniambie nyinyi ni akina nani. Mtume wa Mwenyezi Mungu, swallallahu alayhi wasallam, akasema: «Ukitueleza, tutakueleza» Akasema: Hiyo ni sawa na hiyo? Akasema: «Ndio» Yule mzee akasema: Nimeambiwa kwamba Muhammad na masahaba zake walitoka siku fulani, na ikiwa yule aliyeniambia anasema kweli, wao leo wako mahali fulani kwa mahali ambapo Mtume wa Mwenyezi Mungu, swallallahu alayhi wasallam, alikuwa, na nimeambiwa kwamba Maquraishi walitoka siku fulani, na ikiwa yule aliyeniambia anasema kweli, wao leo wako mahali fulani, kwa mahali ambapo Maquraishi walikuwa, alipomaliza habari zake, akasema: Nyinyi ni akina nani? Mtume wa Mwenyezi Mungu, swallallahu alayhi wasallam, akasema: «Sisi ni kutoka kwa maji». Kisha akaondoka kwenda zake. Anasema yule mzee: Ni maji gani? Je, ni kutoka kwa maji ya Iraq? 

Enyi Waislamu: 

Hivi ndivyo inavyopasa kuwa akili ya muumini, akili ya Kiislamu. Anaelewa mambo, yaani, anatoa hukumu juu yake kulingana na kanuni anayoiamini na kutulia nayo. Na anasifika kwa busara na akili, naye ni mwepesi wa kufahamu, anajitahidi kwa hekima, akijibu jibu la kumnyamazisha adui yake, wala si Mtume, swallallahu alayhi wasallam, peke yake ndiye mwenye akili hii ya Kiislamu, bali masahaba, Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao wote, na haswa Khalifa wa kwanza Abu Bakr As-Siddiq, Radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie, wana akili kama hii, vipi sivyo ilhali wamelelewa katika shule ya utume?

As-Siddiq, Radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie, alifuatana na Mtume wa Mwenyezi Mungu, swallallahu alayhi wasallam, katika hijra yake kutoka Makka kwenda Madina. Naye anajua kwamba maana ya urafiki huu ni kwamba atakuwa peke yake akifuatana na Mtume wa Mola Mlezi wa walimwengu kwa angalau siku kumi na chache, naye ndiye atakayetoa maisha yake kwa bwana wake na kiongozi wake na mpenzi wake Mtume Mustafa, swallallahu alayhi wasallam, ni ushindi gani katika ulimwengu huu unaozidi ushindi huu? Kwamba As-Siddiq atakuwa peke yake bila ya watu wa ardhini, na bila ya masahaba wote akifuatana na Bwana wa viumbe na urafiki wake kwa muda wote huu? Na maana za mapenzi katika Mwenyezi Mungu zinaonekana katika hofu ya Abu Bakr akiwa ndani ya pango kwamba washirikina watamuona, ili As-Siddiq awe mfano wa kile ambacho askari mwaminifu wa da'wa anapaswa kuwa, pamoja na kiongozi wake mwaminifu, wakati hatari inamzunguka kwa hofu na huruma kwa maisha yake, kwani Abu Bakr wakati huo hakuwa anachelea kifo kwa nafsi yake, na lau angekuwa hivyo hangalifuatana na Mtume wa Mwenyezi Mungu, swallallahu alayhi wasallam, katika hijra hii hatari, naye anajua kwamba malipo yake madogo ni kuuliwa ikiwa washirikina watamkamata pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu, swallallahu alayhi wasallam, lakini alikuwa anaogopa uhai wa Mtume mtukufu, swallallahu alayhi wasallam, na mustakabali wa Uislamu ikiwa Mtume, swallallahu alayhi wasallam, angeangukia mikononi mwa washirikina, na hisia kubwa ya kiusalama ya As-Siddiq inaonekana katika hijra yake na Mtume, swallallahu alayhi wasallam, katika hali nyingi, ikiwemo, alipomjibu yule muulizaji: Huyu ni nani huyu mtu aliye mbele yako? Abu Bakr, Radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie, akasema: Huyu ni muongozaji ananiongoza njia, yule muulizaji akadhani kwamba As-Siddiq anamaanisha njia, lakini alikuwa anamaanisha njia ya kheri, na hili linaashiria matumizi mazuri ya Abu Bakr ya maonyesho, akiepuka aibu au uongo, na linaashiria wazi akili ya Kiislamu anayoifurahia.

Enyi Waislamu: 

Je, wanawake wameshindwa kuzaa watu kama hawa wenye akili timamu za Kiislamu? Ili kujibu, tunasema: Hakika mama waliowazaa watu hawa wenye akili timamu za Kiislamu, bado wana uwezo wa kuzaa viongozi wakuu kama hawa ambao sisemi kwa kupita kiasi: Kwamba wao ni kama masahaba, Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao! Na tutatoa mfano hai kutoka katika zama zetu tunazoishi, na nilikuwa shahidi wa macho, ninazieleza kwa uaminifu kama nilivyozishuhudia kwa uhalisia: Wakati Mwenyezi Mungu alinishushia heshima ya kuibeba da'wa pamoja na vijana wa Hizb ut-Tahrir, na nilikamatwa mwaka themanini na tatu, na vyombo vya ujasusi katika jimbo la Jordan, na nilikuwa mgeni kwa da'wa, niliwajua vijana wengi wa chama, na nilijifunza kutoka kwao na kutoka kwa msimamo wao wa ujasiri na ushujaa mambo mengi. Na miongoni mwa vijana hawa mashuhuri niliowajifunza kutoka kwao, na nimenufaika nao faida kubwa ni Amir wetu wa sasa, Amir wa Hizb ut-Tahrir Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah, Mwenyezi Mungu amuhifadhi na amlinde. Hakika yeye ni mwanamume na mwanamume yeyote! Mtu wa aina yake, mwenye tabia ya Kiislamu ya hali ya juu, mwenye akili ya Kiislamu iliyoangaziwa, na mwenye saikolojia ya Kiislamu miongoni mwa saikolojia bora zaidi. Na huu ni ushahidi wa haki nitakao ulizwa juu yake siku ya Qiyama, ninautoa kwa ajili ya uso wa Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu, na ni ushahidi ninaoutoa na kuuwakilisha kwa umma wa Kiislamu, ili huenda ukaongozwa kwa jambo lake la busara zaidi, na linapogusa njia yake kuelekea kwenye utukufu, na linatafuta kiongozi wa kuliongoza kwenye nchi ya amani! Na analihukumu kwa sheria ya Mola Mlezi wake Rahman! Na anatekeleza ndani yake mwongozo wa Qur'an, na anafanya ndani yake sunna ya Nabii Adnan, swallallahu alayhi wasallam. 

Enyi Waislamu: 

Nitawakumbusha msimamo mmoja kutoka kwa misimamo mingi ambayo inaonyesha akili ya hali ya juu ya Kiislamu ambayo Amir wetu Amir wa Hizb ut-Tahrir anafurahia, alitoa hotuba akiwa Amman kwa moyo, na alikuwa akiitoa kana kwamba anasoma kutoka kwa kitabu. Na hotuba hii ilikuwa na kichwa: "Mizozo ya Kiuchumi: Uhakika wake na suluhisho lake kutoka kwa mtazamo wa Uislamu" Na baada ya kuimaliza, alitoa fursa ya kuuliza maswali kutoka kwa waliohudhuria. Hata hivyo, vyombo vya ujasusi vilikuwa vimemdunisha mmoja wa washirika wao ili kuharibu hali ya hotuba, hivyo aliharakisha na kuleta swali lifuatalo: Hizb ut-Tahrir ilianzishwa mwanzoni mwa miaka ya hamsini, basi imefanya nini hadi sasa? Basi Abu Yasin alimjibu nini? Fungueni mioyo yenu na akili zenu enyi waumini na sikilizeni, ili kusikia jibu hili linaloonyesha kasi ya kufahamu kwake, Abu Yasin, Mwenyezi Mungu amuhifadhi na amlinde, alisema: "Nimetoa yale niliyokabidhiwa nayo, na asante". Mara tu wahudhuriaji waliposikia jibu hilo, wote waliokuwa ukumbini waliangua kupiga makofi wakivutiwa nalo.

 Wasikilizaji wapenzi: Wasikilizaji wa redio ya afisi ya habari ya Hizb ut-Tahrir: 

Tunatosheka na kiwango hichi katika kipindi hichi, ili tukamilishe tafakuri zetu katika vipindi vijavyo InshaAllah Ta'ala, mpaka wakati huo na mpaka tutakapokutana nanyi, tunawaacha katika uangalizi wa Mwenyezi Mungu na hifadhi yake na amani yake. Tunawashukuru kwa usikilizaji wenu mzuri na Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh. 

More from null

Tafakuri Katika Kitabu: "Miongoni mwa Sifa za Kisaikolojia za Kiislamu" - Kipindi cha Kumi na Tano

Tafakuri Katika Kitabu: "Miongoni mwa Sifa za Kisaikolojia za Kiislamu"

Maandalizi ya Ustadhi Muhammad Ahmad Al-Nadi

Kipindi cha Kumi na Tano

Alhamdulillah, Mola Mlezi wa walimwengu, na sala na salamu zimwendee imamu wa wachamungu, na bwana wa mitume, aliyetumwa kuwa rehema kwa walimwengu, Bwana wetu Muhammad na ahli zake na masahaba zake wote, na tujaalie kuwa pamoja nao, na utukusanye katika kundi lao kwa rehema yako, Ee Mwenye kurehemu zaidi ya wote wanaorehemu.

Wasikilizaji wapendwa, wasikilizaji wa Radio ya Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir:

Assalamu alaykum warahmatullahi wabarakatuh, ama baada ya hayo: Katika kipindi hiki tunaendelea na tafakuri zetu katika kitabu: "Miongoni mwa Sifa za Kisaikolojia za Kiislamu". Na kwa ajili ya kujenga haiba ya Kiislamu, pamoja na kuzingatia akili ya Kiislamu na saikolojia ya Kiislamu, tunasema na kwa msaada wa Mwenyezi Mungu: 

Enyi Waislamu:

Tulisema katika kipindi kilichopita: Pia ni sunna kwa Muislamu kumuombea ndugu yake kwa siri, kama ilivyo sunna kwake kumuomba ndugu yake amwombee, na ni sunna kwake kumtembelea na kuketi naye na kuendeleza uhusiano naye na kutoa mali yake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu baada ya kumpenda. Na ni vizuri kwa Muislamu kumlaki ndugu yake kwa yale anayopenda ili kumfurahisha kwa hayo. Na tunaongeza katika kipindi hiki kwa kusema: Hakika ni vizuri kwa Muislamu kumpa zawadi ndugu yake, kwa hadithi ya Abu Hurairah ambayo Bukhari ameitoa, katika Adab al-Mufrad, na Abu Ya'la katika Musnad yake, na al-Nasa'i katika Al-Kuna, na Ibn Abd al-Barr katika Al-Tamhid, na al-Iraqi alisema: Mnyororo wa wapokezi ni mzuri, na Ibn Hajar alisema katika Al-Talkhis al-Habir: Mnyororo wake wa wapokezi ni mzuri, alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, swallallahu alayhi wa sallam, amesema: "Peaneneni zawadi, mtapendana." 

Na ni vizuri pia kwake kuikubali zawadi yake, na kumlipa kwa zawadi hiyo, kwa hadithi ya Aisha kwa Bukhari, alisema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu, swallallahu alayhi wa sallam, alikuwa akipokea zawadi na kulipa kwa hiyo."

Na hadithi ya Ibn Omar kwa Ahmad na Abu Dawood na al-Nasa'i, alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, swallallahu alayhi wa sallam, amesema: "Yeyote anayeomba hifadhi ya Mwenyezi Mungu, basi mpeni hifadhi, na yeyote anayewaomba kwa jina la Mwenyezi Mungu, basi mpeni, na yeyote anayewaomba ulinzi wa Mwenyezi Mungu, basi mkingeni, na yeyote anayewafanyia wema, basi mlipe, na ikiwa hamupati, basi mwombeeni mpaka mjue kwamba mmemlipa."

Hii ni kati ya ndugu, na haina uhusiano wowote na zawadi za raia kwa watawala, kwani ni haramu kama rushwa, na miongoni mwa malipo ni kusema: Mwenyezi Mungu akulipe kheri. 

Tirmidhiy amepokea kutoka kwa Usama bin Zaid, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, na akasema ni hadithi nzuri na sahihi, alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, swallallahu alayhi wa sallam, amesema: "Yeyote anayefanyiwa wema, na akamwambia aliyemfanyia: "Mwenyezi Mungu akulipe kheri", basi amekamilisha sifa." Na sifa ni shukrani, yaani malipo, hasa kutoka kwa mtu ambaye hapati chochote kingine, kama alivyopokea Ibn Hibban katika Sahih yake kutoka kwa Jabir bin Abdullah, alisema: Nilimsikia Nabii, swallallahu alayhi wa sallam, akisema: "Yeyote anayefanyiwa wema, na hakupata wema wowote isipokuwa sifa, basi amemshukuru, na yeyote anayeuficha, basi ameukufuru, na yeyote anayejipamba kwa uongo, basi ni kama amevaa nguo mbili za uongo." Na kwa isnadi nzuri kwa Tirmidhiy kutoka kwa Jabir bin Abdullah, alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: "Yeyote anayepewa zawadi, na akapata cha kulipa, basi alipe kwa hiyo, na ikiwa hapati, basi asifie kwa hiyo, kwa sababu yeyote anayesifia kwa hiyo, basi amemshukuru, na yeyote anayeuficha, basi ameukufuru, na yeyote anayejipamba kwa kile ambacho hakupatiwa, basi ni kama amevaa nguo mbili za uongo." Na kukufuru zawadi kunamaanisha kuificha na kuifunika. 

Na kwa isnadi sahihi, Abu Dawood na al-Nasa'i wamepokea kutoka kwa Anas, alisema: "Wahajiri walisema, Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu, Ansari wamechukua ujira wote, hatujawahi kuwaona watu wazuri zaidi katika kutoa kwa wingi, wala wazuri zaidi katika kuhurumiana katika uchache kuliko wao, na wametuondolea mzigo, alisema: Je, hamwawasifu kwa hilo na kuwaombea? Walisema: Ndio, alisema: Basi hiyo ni kwa hiyo." 

Na inampasa Muislamu kushukuru kidogo kama anavyoshukuru kingi, na kuwashukuru watu wanaomfanyia wema, kama alivyopokea Abdullah bin Ahmad katika Zawaid yake kwa isnadi nzuri kutoka kwa al-Nu'man bin Bashir, alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, swallallahu alayhi wa sallam, amesema: "Yeyote asiyeshukuru kidogo, hatashukuru kingi, na yeyote asiyewashukuru watu, hatamshukuru Mwenyezi Mungu, na kuzungumzia neema ya Mwenyezi Mungu ni shukrani, na kuiacha ni kufuru, na jamaa ni rehema, na utengano ni adhabu."

Na miongoni mwa sunna ni kumuombea ndugu yake kwa manufaa ya wema au kurahisisha magumu, kama alivyopokea Bukhari kutoka kwa Abu Musa, alisema: "Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, alikuwa ameketi pale alipokuja mtu akiuliza, au akihitaji haja, akatuelekeza uso wake na akasema ombeeni ili mthawabishwe na Mwenyezi Mungu atimize kwa ulimi wa nabii wake atakavyo."

Na kama alivyopokea Muslim kutoka kwa Ibn Omar kutoka kwa Nabii, swallallahu alayhi wa sallam, alisema: "Yeyote aliyekuwa kiungo kwa ndugu yake Muislamu kwa mwenye mamlaka kwa manufaa ya wema au kurahisisha magumu, atasaidiwa kupita Siraati siku ya kuteleza miguu."

Na ni vizuri pia kwa Muislamu kulinda heshima ya ndugu yake kwa siri, kama alivyopokea Tirmidhiy na akasema hii ni hadithi nzuri kutoka kwa Abu al-Darda' kutoka kwa Nabii, swallallahu alayhi wa sallam, alisema: "Yeyote anayerudisha (anayetetea) heshima ya ndugu yake, Mwenyezi Mungu atarudisha moto kutoka usoni mwake Siku ya Kiyama." Na hadithi hii ya Abu al-Darda' ameitoa Ahmad na akasema isnadi yake ni nzuri, na vile vile alisema al-Haythami. 

Na kama alivyopokea Ishaq bin Rahwayh kutoka kwa Asma binti Yazid, alisema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu, swallallahu alayhi wa sallam, akisema: "Yeyote anayetetea heshima ya ndugu yake kwa siri, ni haki kwa Mwenyezi Mungu kumwacha huru na moto." 

Na al-Quda'i ameitoa katika Musnad al-Shihab kutoka kwa Anas, alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, swallallahu alayhi wa sallam, amesema: "Yeyote anayemsaidia ndugu yake kwa siri, Mwenyezi Mungu atamsaidia katika dunia na akhera." Na al-Quda'i pia ameitoa kutoka kwa Imran bin Hussein kwa ziada: "Naye anaweza kumsaidia." Na kama alivyopokea Abu Dawood na Bukhari katika Al-Adab al-Mufrad, na al-Zain al-Iraqi alisema: Isnad yake ni nzuri kutoka kwa Abu Hurairah kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu, swallallahu alayhi wa sallam, amesema: "Muumini ni kioo cha muumini, na muumini ni ndugu wa muumini, kokote anapokutana naye, anazuia kupotea kwake na anamzunguka nyuma yake."

Enyi Waislamu:

Mmejua kupitia hadithi za Nabii tukufu zilizotajwa katika kipindi hiki, na kipindi kilichopita, kwamba ni sunna kwa yule anayempenda ndugu yake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kumjulisha na kumueleza upendo wake kwake. Na pia ni sunna kwa Muislamu kumuombea ndugu yake kwa siri. Kama ilivyo sunna kwake kumuomba ndugu yake amwombee. Na ni sunna kwake kumtembelea na kuketi naye na kuendeleza uhusiano naye na kutoa mali yake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu baada ya kumpenda. Na ni vizuri kwa Muislamu kumlaki ndugu yake kwa yale anayopenda ili kumfurahisha kwa hayo. Na ni vizuri kwa Muislamu kumpa zawadi ndugu yake. Na ni vizuri pia kwake kuikubali zawadi yake, na kumlipa kwa zawadi hiyo.

Na inampasa Muislamu kuwashukuru watu wanaomfanyia wema. Na miongoni mwa sunna ni kumuombea ndugu yake kwa manufaa ya wema au kurahisisha magumu. Na ni vizuri pia kwake kulinda heshima ya ndugu yake kwa siri. Je, hatutazifuata hukumu hizi za kisheria, na hukumu zingine za Uislamu; ili tuwe kama anavyopenda na kuridhika Mola wetu, mpaka abadilishe yaliyomo ndani yetu, na atengeneze hali zetu, na tupate ushindi wa kheri za dunia na akhera?! 

Wasikilizaji wapendwa: Wasikilizaji wa Radio ya Ofisi ya Habari ya Hizb ut-Tahrir: 

Tunatosheka na kiasi hiki katika kipindi hiki, tukitarajia kukamilisha tafakuri zetu katika vipindi vijavyo, InshaAllah Ta'ala, mpaka wakati huo na mpaka tukutane, tunawaacha katika uangalizi wa Mwenyezi Mungu na ulinzi wake na usalama wake. Tunawashukuru kwa usikilizaji wenu mzuri na Assalamu alaykum warahmatullahi wabarakatuh. 

Fahamuni Enyi Waislamu! - Kipindi cha 15

Fahamuni Enyi Waislamu!

Kipindi cha 15

Kwamba miongoni mwa vyombo vya dola ya Khilafa ni wasaidizi, nao ni mawaziri ambao Khalifa huwateua pamoja naye, ili wamsaidie katika kubeba majukumu ya Khilafa, na kutekeleza majukumu yake, kwa sababu wingi wa majukumu ya Khilafa, haswa kila inapokua na kupanuka dola ya Khilafa, Khalifa hulemewa na kuyabeba peke yake, hivyo anahitaji mtu wa kumsaidia katika kuyabeba ili atekeleze majukumu yake, lakini haifai kuwaita mawaziri bila ya kizuizi mpaka isije ikachanganya maana ya waziri katika Uislamu ambayo ni sawa na msaidizi na maana ya waziri katika mifumo ya kidunia ya sasa kwa misingi ya kidemokrasia, kibepari, kilimwengu au mifumo mingine ambayo tunaishuhudia katika zama hizi za sasa.