Msururu wa "Ukhalifa na Uimamu katika Fikra ya Kiislamu"
Mwandishi na Mwanafikra Thair Salama – Abu Malik
Sehemu ya Nne: Kusimamisha Ukhalifa ni miongoni mwa Makusudio Makuu ya Sharia Sehemu ya 2
Na wanachuoni wamebainisha makusudio manane1 muhimu kwa mwanadamu nayo ni: kuhifadhi nafsi, mali, dini, akili, kizazi, kuhifadhi dola, kuhifadhi usalama na kuhifadhi heshima ya kibinadamu, na tunaweza kuongeza kwake makusudio makuu yaliyobainishwa kutoka katika aya hizi: kusimamisha uadilifu, kutekeleza sheria, huruma, ibada, uongofu na kubainisha hukumu.
Basi dini kwa hakika: imeteremshwa ili iwe mfumo wa maisha ambao unawahukumu watu kwa hukumu zake katika maisha yao kwa wajibu2, ﴿WANADAMU WALIKUWA UMMAT MMOJA, ALLAH AKAWAPELEKEA NABII KUWA WA BASHIRI NA WA ONYO NA AKATEREMSHA PAMOJA NAO KITABU KWA HAKI ILI HUKUMU KATI YA WATU KATIKA YALE WANAYOTOFATIANA﴾ [Al-Baqara: 213], na lamu katika kauli yake ﴿ILI HUKUMU KATI YA WATU﴾ ni lamu ya sababu, basi moja ya makusudio muhimu ya ujumla ya kupelekwa Manabii na pamoja nao bishara na onyo ni kwamba Kitabu kihukumu baina ya watu ili kuboresha maisha yao na haki na uadilifu vitawale katika kila jambo la mambo yao ya maisha!, na kwa hiyo basi kutekelezwa kwa hukumu hizi katika uhalisia wa maisha hakika ni makusudio makuu ya sharia, na makusudio ya kutumwa Mtume ﷺ, na makusudio ya kuteremshwa Kitabu! na msingi wa dini imara, na kusimamisha kwake katika maisha ya watu hakika ni miongoni mwa wajibu ulio muhimu zaidi, basi kusimamisha dola ya Kiislamu, yaani dola ya Ukhalifa ni njia ambayo kupitia kwake yanatimizwa makusudio ambayo kwa ajili yake Allah amemtumwa Mtume ﷺ, na ambayo kwa ajili yake ameteremsha Kitabu!
Na vinginevyo basi Uislamu si falsafa ya kufikirika, bali umeteremshwa ili utekelezwe na uhukumu, na imethibitishwa kwamba hukumu hizi hakika zinasimamishwa katika maisha ya Waislamu kupitia dola inayoongoza3, inayoendeshwa na mfumo wa hukumu uliopangwa kisheria ambao Mtume ﷺ ameiita dola ya Ukhalifa4, na akaisimamisha kivitendo, na akasimamisha taasisi zake, na sheria zake, ikapatikana dola kweli, na haikuwa miongoni mwa jambo la Masahaba kuelekea kwake ila kuendeleza yale aliyoanza Bwana wa viumbe ﷺ kuhusu hilo, basi ni dola ambayo nguzo zake zimeegemea kwenye kitendo cha Mtume ﷺ, na kwenye hukumu ambazo zinawakilisha wingi wa Qur'an na Sunnah ambazo ziliteremshwa ili zitekelezwe kupitia kwake, ambazo Masahaba wamekubaliana juu ya ulazima wake kwa ijmai yao, na ulazima wake umeenea kwa njia ya maana, na hawezi kulijua jambo kama hilo la dola kuwepo na hukumu na taasisi, au kusema kuwa ni mfumo wa kibinadamu usio lazima ila mjinga!
1- Imamu Shatibi amebainisha makusudio matano muhimu: nayo ni kuhifadhi nafsi, mali, dini, akili na kizazi, na ameongeza kwake Imamu Taqiuddin Nabhani makusudio ya kuhifadhi usalama, na makusudio ya kuhifadhi dola, na makusudio ya kuhifadhi heshima ya kibinadamu, kwa kuyabainisha kupitia ukali wa adhabu kwa mtendaji wa uhalifu unaoyagusa kisheria, basi anayetoka nje ya dola kwa silaha anapigwa vita, na anayepasua fimbo ya utiifu na kuapa bay'a kwa Khalifa wa pili anauawa, na mengineyo katika hukumu na maelezo marefu marejeo yake ni kitabu cha haiba ya Kiislamu juzuu ya tatu, yakawa makusudio muhimu ni manane.
2- Hakika faradhi ya Swala, na faradhi ya Zaka ni miongoni mwa faradhi kubwa za Uislamu, lakini faradhi bila ya kutekelezwa, inasababisha adhabu kali, kwa sababu faradhi na hukumu zingine hakika zimeteremshwa ili zitekelezwe na kufanyiwa kazi, basi Uislamu si falsafa ya kufikirika, wala jamhuri zilizo bora, bali ni hukumu zilizoteremshwa kwa ajili ya utekelezaji, na hakika imesimama dola katika Uislamu, na imefaradhishwa Ukhalifa na Muumbaji, kwa sababu kupitia kwake kuna utekelezaji wa faradhi zote na wajibu na hukumu, bali zaidi ya 90% ya hukumu za Uislamu! Na Abu Bakr radhi za Allah ziwe juu yake alilifahamu hilo kwa ufahamu wa kweli kwani alisema: Wallahi nitawapiga vita wanaotenganisha baina ya Swala na Zaka, kwani Zaka ni haki ya mali, Wallahi lau wangenizuia kamba ya ngamia walikuwa wakimlipa Mtume wa Allah ningewapiga vita kwa kuzuia kwake. Basi alipigana kwa sifa yake ya kuwa Khalifa wa Waislamu na aliyemzuia Zaka, basi Zaka inatolewa kwake yeye yaani kwa Sultan!
3- Rejea kitabu chetu: Je, Mtume ﷺ alibainisha njia ya kusimamisha dola ya Kiislamu, basi ndani yake kuna maelezo marefu na dalili imara kwamba Mtume ﷺ alikuwa akifanya kazi ya kuleta dola, na anasema Ibn Taymiyyah katika kitabu cha Siasa ya Kisharia uk. 114 na Majmu'u al-Fatawa j 28/ uk 390: Inawajibika kujua kwamba watawala wa mambo ya watu ni miongoni mwa wajibu mkubwa wa dini bali hakuna usimamaji wa dini ila kwao kwani wanadamu hawakamilishi maslahi yao ila kwa kukutana kwa haja ya baadhi yao kwa wengine na ni lazima kwao wakati wa kukutana kuwa na haja ya kichwa. Na alisema Dkt. Dhiyauddin al-Rais katika kitabu chake Uislamu na Ukhalifa uk 99: "Basi Ukhalifa ni wadhifa muhimu wa kidini na unaowahusu Waislamu wote, na hakika sharia ya Kiislamu imeeleza kwamba kusimamisha Ukhalifa ni faradhi ya msingi miongoni mwa faradhi za dini bali ni faradhi iliyo kuu zaidi kwa sababu utekelezaji wa faradhi zingine unategemea kwake" Angalia: Tanbihi ya wenye kusahaulika na uelezaji kwa wenye kuchanganyikiwa kwamba kurejesha Ukhalifa ni miongoni mwa wajibu mkubwa wa dini hii kwa Sheikh Ali Bin Hajj.
4- Katika Sunan Abu Daud na ameisahihisha Albaani «ametuhadithia Ahmad Bin Swaleh ametuhadithia Asad Bin Musa ametuhadithia Muawiya Bin Swaleh amenihadithia Dhamra kwamba Ibn Zughb al-Ayadi amemuhadithia akasema alishuka juu yangu Abdullah Bin Hawala al-Azdi akasema kwangu: ametutuma Mtume wa Allah ﷺ ili tupate ngawira kwa miguu yetu tukarudi hatukupata ngawira chochote na AKAJUA taabu katika nyuso zetu akasimama kwetu akasema: Ewe Allah usiwakabidhi kwangu nika dhaifu kuwatosheleza wala usiwakabidhi kwa nafsi zao wenyewe wakashindwa kuimudu wala usiwakabidhi kwa watu wakajichukulia wao kisha akaweka mkono wake juu ya kichwa changu au akasema juu ya utosi wangu kisha akasema: Ewe Ibn Hawala ukiona Ukhalifa umeshuka ardhi Takatifu hakika zimekaribia tetemeko na balaa na mambo makubwa, na Saa siku hiyo ni karibu zaidi kwa watu kuliko mkono wangu huu kwa kichwa chako, akasema Abu Daud Abdullah Bin Hawala ni Homsi»; na amesema Muslim: «ametuhadithia Huddab Bin Khalid al-Azdi ametuhadithia Hammad Bin Salama kutoka kwa Samak Bin Harb akasema: nimemsikia Jabir Bin Samura akisema: nimemsikia Mtume wa Allah ﷺ akisema: "Uislamu utazidi kuwa mtukufu mpaka makhalifa kumi na wawili»; kutoka kwa al-Irbadh Bin Sariya akasema: «kisha akatupa mawaidha Mtume wa Allah ﷺ siku moja baada ya Swala ya Alfajiri mawaidha yenye kufika sana macho yakabubujika na nyoyo zikaogopa, akasema mtu: Hakika haya ni mawaidha ya kuaga, basi unatuahidi nini kwetu ewe Mtume wa Allah? Akasema: ninakusieni kumcha Allah na kusikia na kutii hata kama mtumwa mweusi, kwani atakayeishi miongoni mwenu ataona tofauti nyingi, na tahadharini na mambo ya kuzua kwani ni upotevu, atakayelipata hilo miongoni mwenu basi ni juu yenu kushikamana na Sunnah zangu na Sunnah za Makhalifa Waongofu waongozwa mshikamane nayo kwa magego»; Na amesimulia Muslim kutoka kwa Furat al-Qazzaz kutoka kwa Abu Hazim akasema: «nilikaa na Abu Huraira miaka mitano nikamsikia akihadithia kutoka kwa Mtume ﷺ akasema "watu wa Israel walikuwa wanawaongoza Manabii kila alipokufa Nabii alifuatwa na Nabii na hakika hakuna Nabii baada yangu na watakuwepo Makhalifa watakuwa wengi wakasema basi unatuamrisha nini akasema timizeni bay'a ya wa kwanza kisha wa kwanza na wapeni haki yao kwani Allah atawauliza kuhusu yale aliyowachunga»; «utakuwepo Utume kwenu atakavyo Allah kuwepo, kisha ataunyanyua Allah atakavyo kuunyanyua, kisha utakuwepo Ukhalifa juu ya njia ya Utume, utakuwepo atakavyo Allah kuwepo, kisha ataunyanyua Allah atakavyo kuunyanyua, kisha utakuwepo ufalme wa kuumana, utakuwepo atakavyo Allah kuwepo, kisha ataunyanyua Allah atakavyo kuunyanyua, kisha utakuwepo ufalme wa kidhalimu, utakuwepo atakavyo Allah kuwepo, kisha ataunyanyua atakavyo kuunyanyua, kisha utakuwepo Ukhalifa juu ya njia ya Utume, kisha akanyamaza». Na hadithi hii ni nzuri ameitoa Ahmad (30/355 hadithi 18406), na al-Bazzar na al-Twabarani katika al-Awsat (6577) na sanad ya Ahmad ni nzuri ndani yake Daud Bin Ibrahim al-Wasiti amesimulia kutoka kwake al-Twyalisi na akamthibitisha na amemtaja Ibn Hibban katika wathika. Na ameisimulia hadithi pia al-Twyalisi na al-Baihaqi katika Minhaj al-Nubuwa, na al-Twabari, na hadithi ameisahihisha Albaani katika Silsila Sahihi, na ameihasanisha al-Arna'ut, na hadithi ina ushahidi kutoka kwa Safina radhi za Allah ziwe juu yake, akasema: Amesema Mtume wa Allah ﷺ: «UKHALIFA KATIKA UMMAT WANGU NI MIAKA THELATHINI, KISHA UFALME BAADA YA HAPO». KISHA AKASEMA SAFINA: SHIKILIA KWAKO UKHALIFA WA ABU BAKR, KISHA AKASEMA: NA UKHALIFA WA UMAR NA UKHALIFA WA UTHMAN, KISHA AKASEMA KWANGU: SHIKILIA UKHALIFA WA ALI akasema: TUKAPATA MIAKA THELATHINI. Ameisimulia Ahmad na amehusanisha al-Arna'ut. Na amesimulia Imamu Ahmad kutoka kwa Hudhaifa radhi za Allah ziwe juu yake kwamba alisema: "umeondoka Utume ukawepo Ukhalifa juu ya njia ya Utume". Na ameusahihisha al-Arna'ut.