Tafakari Katika Kitabu: "Miongoni mwa Misingi ya Saikolojia ya Kiislamu"
Sehemu ya Saba
Himdi ni ya Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu, na sala na salamu zimwendee imamu wa wachamungu, na bwana wa mitume, aliyetumwa kuwa rehema kwa walimwengu, bwana wetu Muhammad na kwa Aali zake na Masahaba zake wote, na utujaalie kuwa pamoja nao, na utukusanye katika kundi lao kwa rehema yako Ewe Mwingi wa Rehema.
Wasikilizaji wangu wapendwa, wasikilizaji wa redio ya Ofisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir:
Asalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh, Ama baada ya hayo:
Katika sehemu hii tunaendelea na tafakari zetu katika kitabu: "Miongoni mwa Misingi ya Saikolojia ya Kiislamu". Na kwa ajili ya kujenga haiba ya Kiislamu, pamoja na kuzingatia akili ya Kiislamu na saikolojia ya Kiislamu, tunasema na kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu:
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {NA KIMBIENI KWENYE MAGHFIRA KUTOKA KWA MOLA WENU MLEZI, NA PEPONI AMBAYO UPANA WAKE NI MBINGU NA ARDHI, ILIYOANDALIWA KWA AJILI YA WACHAMUNGU}. (Aali Imran 133).
Na akasema: {KAULI YA WAUMINI WANAPOITWA KWA MWENYEZI MUNGU NA MTUME WAKE ILI AWAHUKUMU BAINA YAO, NI KUSEMA: TUMESIKIA NA TUMET'II. NA HAO NDIO WENYE KUFANIKIWA. (51) NA ANAYEMT'II MWENYEZI MUNGU NA MTUME WAKE, NA AKAMKHUSHU MWENYEZI MUNGU, NA AKAMCHA, BASI HAO NDIO WALIOFAULU}. (An-Nur 51-52).
Na akasema: {HAIFAI MUUMINI MWANAMUME WALA MUUMINI MWANAMKE, ALLAH NA MTUME WAKE WANAPOKATA SHAUIRI, WAWE NA HAKI YA KUCHAGUA KATIKA SHAURI YAO. NA ANAYEMUASI ALLAH NA MTUME WAKE, BASI AMEPOTEA UPOTEVU ULIO WAZI}. (Al-Ahzab 36).
Na akasema: {LA, NAAPA KWA MOLA WAKO MLEZI! HAWAWEZI KUWA WAUMINI HATA WAKUFANYE WEWE HUKUMU KATIKA YALE WANAYOZOZANA, KISHA WASIPATE NYOYONI MWAO CHOYO KWA UAMUZI WAKO, NA WAJISALIMISHE KABISA}. (An-Nisa 65).
Na akasema: {ENYI MLIOAMINI! JILINDENI NAFSI ZENU NA FAMILIA ZENU NA MOTO AMBAO KUNI ZAKE NI WATU NA MAWE. WANAUSIMAMIA MALAIKA WAKALI, WENYE NGUVU, HAWAMUASI ALLAH KWA ANAYO WAAMRISHA, NA WANAFANYA WANAYOAMRISHWA}. (At-Tahrim 6).
Na amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ: «Fanyeni haraka matendo kabla ya fitna kama vipande vya usiku wenye giza mtu huamkia akiwa muumini na hufika jioni akiwa kafiri, na hufika jioni akiwa muumini na huamkia akiwa kafiri anauza dini yake kwa manufaa ya dunia» Imepokewa na Muslim kutoka kwa Abu Hurairah.
Enyi Waislamu:
Hakika wale wanaokimbilia msamaha na pepo na kufanya haraka matendo mema walipatikana katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ, na katika karne zilizofuata, na umma ungali unazaa hawa wanaokimbilia ambao wanamuitikia Mola wao na wanajitoa nafsi zao kwa ajili ya kutafuta radhi zake, na miongoni mwa hayo ni:
Katika hadithi ya Jabir iliyokubaliwa alisema: «Alimwambia mtu Mtume ﷺ siku ya Uhud: Unasemaje nikiuawa niko wapi? Alisema: Peponi, akatupa tende zilizokuwa mkononi mwake kisha akapigana mpaka akauliwa». Na hadithi ya Anas kwa Muslim na ndani yake: «Akaondoka Mtume ﷺ na Masahaba zake mpaka wakawatangulia washirikina kwenda Badr na wakaja washirikina, akasema Mtume ﷺ: Simameni kwenye pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, akasema Umayr bin al-Hammam al-Ansari: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi? Akasema: Ndio, akasema: Bakhi Bakhi, akasema Mtume ﷺ: Nini kinachokufanya useme Bakhi Bakhi? Akasema: La wallahi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu isipokuwa natarajia kuwa mimi ni miongoni mwa watu wake, akasema: Hakika wewe ni miongoni mwa watu wake, akatoa tende kutoka kwenye mfuko wake, akaanza kula, kisha akasema: Ikiwa nitaishi mpaka nile tende zangu hizi hakika huo ni uhai mrefu, akasema: Akatupa aliyokuwa nayo ya tende, kisha akapigana nao mpaka akauliwa».
Na katika hadithi ya Anas iliyokubaliwa alisema: «Alikosekana ami yangu Anas bin an-Nadr katika vita vya Badr, akasema ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nimekosekana katika vita vya kwanza ulivyopigana na washirikina, ikiwa Mwenyezi Mungu atanishuhudisha vita na washirikina, Mwenyezi Mungu ataona nitakachokifanya, ilipokuwa siku ya Uhud, na Waislamu walipokimbia, akasema: Ewe Mwenyezi Mungu mimi nakuomba radhi kutokana na yale waliyoyafanya hawa, yaani Masahaba, na ninajitenga na yale waliyoyafanya hawa yaani washirikina, kisha akasonga mbele akakutana na Saad bin Muadh, akasema: Ewe Saad bin Muadh pepo naapa kwa Mola wa an-Nadr, mimi ninaisikia harufu yake kutoka upande wa Uhud, akasema Saad sikuweza ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu alichokifanya? Akasema Anas: Tukapata kwake mapigo themanini na kitu kwa upanga au kuchomwa kwa mkuki au kurushiwa kwa mshale, na tukampata ameuawa, na washirikina wamemfanyia unyama, hakumjua yeyote isipokuwa dada yake kwa ncha ya kidole chake» akasema Anas tulikuwa tunaona au tunadhani kuwa aya hii ilishushwa kumhusu yeye na watu mfano wake {KATIKA WAUMINI WAPO WANAUME WALIOKUWA WA KWELI KATIKA YALE WALIOAHIDIANA NA ALLAH}. (Al-Ahzab 23) mpaka mwisho wa aya.
Enyi Waislamu:
Imepokewa na Bukhari kutoka kwa Abu Sarwa'a alisema: «Nimeswali nyuma ya Mtume ﷺ Madina Alasiri akatoa salamu, kisha akasimama kwa haraka, akawaruka watu kwenda kwenye vyumba vya wake zake, watu walishtuka kwa haraka yake, akawatokea, akaona kuwa wamestaajabu kwa haraka yake akasema: Nimekumbuka kitu cha dhahabu tulichokuwa nacho, nimechukia kinizuie, nikaamrisha kigawanywe» na katika riwaya yake: «Nilikuwa nimeacha nyumbani dhahabu kutoka kwa sadaka, nimechukia kuilaza». Na hili linawaongoza Waislamu kwenye kufanya haraka na kuharakisha katika kutekeleza yale ambayo Mwenyezi Mungu amewawajibisha. Na imepokewa na Bukhari kutoka kwa al-Baraa alisema: «Alipokuja Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ Madina aliswali akielekea Bayt al-Maqdis miezi kumi na sita au kumi na saba na alikuwa anapenda aelekezwe kwenye Kaaba Mwenyezi Mungu Mtukufu akateremsha hakika tunaona kugeuka kwa uso wako mbinguni basi tutakuelekeza kibla unachokipenda akaelekezwa kwenye Kaaba akaswali naye mtu alasiri kisha akatoka akapita kwa watu kutoka kwa Ansar akasema yeye anashuhudia kuwa ameswali na Mtume ﷺ na kuwa ameielekea Kaaba wakageuka hali wao wanasujudu katika sala ya Alasiri».
Na imepokewa na Bukhari kutoka kwa Ibn Abi Aufa Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao anasema: «Tulipatwa na njaa katika usiku wa Khaibar ilipokuwa siku ya Khaibar tukaingia kwenye punda wa kufugwa tukawachinja vilipochemka vyungu akaita mtangazaji wa Mtume ﷺ mimineni vyungu msiwale nyama ya punda kitu chochote alisema Abdallah tukasema hakika Mtume ﷺ amekataza kwa sababu haijatolewa khumsi alisema na wengine wameharamisha kabisa na nimemuuliza Said bin Jubair akasema amehairamisha kabisa».
Na imepokewa na Bukhari kutoka kwa Anas bin Malik Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alisema: «Nilikuwa namnywesha Abu Talha al-Ansari na Abu Ubaidah bin al-Jarrah na Ubai bin Kaab kinywaji kutoka kwa fadhiidh nayo ni tende, akawajia mgeni akasema: Hakika ulevi umeharamishwa akasema Abu Talha: Ewe Anas simama kwenye hizi mitungi ivunje, akasema Anas: Nikasimama kwenye kinu chetu nikakipiga chini mpaka kikavunjika».
Na imepokewa na Bukhari kutoka kwa Aisha Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alisema: «Tulifikishiwa kuwa alipoteremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu warejeshe kwa washirikina yale waliyoyatumia kwa wale waliohama kutoka kwa wake zao na akawahukumu Waislamu wasishikamane na ndoa za makafiri kuwa Omar amewapa talaka wake zake wawili». Na imepokewa na Bukhari kutoka kwa Aisha Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alisema: «Mwenyezi Mungu awarehemu wanawake wahajiri wa mwanzo aliposhusha Mwenyezi Mungu {NA WAANZE KUFUNIKA VIFUA VYAO KWA HIJABU ZAO}. Walikata nguo zao wakajifunika nazo».
Enyi Waislamu:
Ikiwa tunataka Mwenyezi Mungu Mtukufu atukirimu kwa nusra yake, na abadilishe hali zetu kuwa yale tunayoyapenda na kuyaridhia, na atutukuze kwa Uislamu, na autukuze Uislamu kwa ajili yetu, kama alivyomkirimu Nabii wake Muhammad ﷺ, na Masahaba zake watukufu Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, na akawashinda maadui zao makafiri, basi hatuna budi isipokuwa kumfuata Nabii wetu, na kufuata nyayo za Masahaba katika haraka ya kuitikia amri ya Mwenyezi Mungu Mkuu.
Wasikilizaji wangu wapendwa: Wasikilizaji wa redio ya Ofisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir:
Tunatosheka na kiasi hiki katika sehemu hii, kwa ajili ya kukamilisha tafakari zetu katika sehemu zijazo In Shaa Allah Taala, mpaka wakati huo na mpaka tutakapokutana nanyi, tunawaacha katika uangalizi wa Mwenyezi Mungu na hifadhi yake na amani yake. Tunawashukuru kwa usikilizaji wenu mzuri na Asalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.