Nafais Al-Thamarati - Fadhila za Subira na Watu Wenye Subira
Mwenyezi Mungu amewasifu wenye subira kwa sifa, na ametaja subira katika Qur'ani katika zaidi ya sehemu sabini na akaongeza kheri nyingi kwake akisema: {NA TUKAWAFANYA MIONGONI MWAO VIONGOZI WANAOONGOZA KWA AMRI YETU WALIPO SUBIRI}, na akasema: {NA LIMETIMIA NENO LA MOLA WAKO MZURI KWA WANA WA ISRAILI KWA WALIVYO SUBIRI}, na akasema: {NA HAKIKA TUTAWALIPA WALE WALIO SUBIRI UJIRA WAO KWA UZURI WA YALE WALIOKUWA WAKIYAFANYA},