Ghadhabu kwa Watu wa Gaza kutoka Ng'ambo Inadai Kuvunjwa kwa Mzingiro... Ni Lini Watu wa Kinana na Jeshi Lao Wataghadhibika? Ni Lini Ghadhabu Yao Itakuwa Moto Utakaochoma Taasisi ya Wayahudi na Mifumo ya Ukoloni Inayoilinda?
Wakati Gaza inakufa kwa njaa, na inazingirwa chini ya ukimya wa aibu wa Kiarabu, na njama ya kimataifa iliyo wazi, kijana Mmisri kutoka ng'ambo, anayeitwa Anas Habib, anafunga milango ya ubalozi wa Misri nchini Uholanzi kwa kufuli, na kumwaga unga kwenye mlango wake, akipaza sauti kwa jina la watu wa Gaza waliozingirwa, na anawaita wana wa jeshi lake huko Misri kuvunja mzingiro, kufungua kivuko, na kukomesha njaa iliyopangwa... Kilio kutoka nchi ya mbali kilisikika katika mioyo huru, je, kuna anayejibu kutoka kwa watu wa Misri? Je, kuna wivu katika mioyo ya askari wa jeshi la Kinana? Au kufuli zilizowekwa kwenye ubalozi wa Misri huko The Hague ni kali kidogo kuliko kufuli zilizowekwa kwenye utashi wao na silaha zao?!