Abu Wadaha News: Taarifa kwa Vyombo vya Habari kutoka Hizb ut-Tahrir Kuhusu Kuvunjwa kwa Masoko Kama Soko la Dukhinat Ni Kupambana na Watu Katika Riziki Zao na Maisha Yao na Ni Matokeo ya Kukosekana kwa Dola ya Kiislamu ya Khilafa
Katika kitendo cha kinyama na cha ukatili, mamlaka za mtaa za Jabal Awliya katika jimbo la Khartoum, kupitia askari wenye silaha nzito asubuhi ya Alhamisi 12/6/2025, waliondoa soko la Dukhinat lililoko katika barabara ya Jabal Awliya, kwa buldoza, na wakavunja meza za maonyesho, na hata wale waliokimbia soko na bidhaa zao hawakuokoka!