Muhtasari wa Habari 07-08-2025
Shirika la Kiyahudi lilitishia kukalia kabisa Ukanda wa Gaza. Mnamo 2025/8/5, ilitangazwa kuwa Waziri Mkuu wake, Netanyahu, alifanya mashauriano kuhusu suala hili na atatangaza uamuzi kuhusu hilo baadaye. Ikumbukwe kwamba kwa miezi 22 amekuwa akifanya kazi ya kuharibu eneo hilo na kuangamiza watu wake, kwani ameharibu zaidi ya 80% ya nyumba, shule na hospitali zao, na anaendelea kuwashambulia watu katika mahema, mitaani, na karibu na vituo vya ugawaji wa misaada. Yeye na jeshi lake hawajashiba damu ya watu wa Gaza.