Rada: Taarifa kwa Vyombo vya Habari.. Sehemu ya Wanawake katika Afisi ya Habari Kuu ya Hizb ut-Tahrir Yazindua Kampeni ya Ulimwengu yenye Kichwa: "Vita vya Sudan: Kisa cha Ukoloni, Usaliti, na Kukata Tamaa"
Vita vya kikatili nchini Sudan kati ya Vikosi vya Wanajeshi vya Sudan vinavyoongozwa na mtawala wa Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, na Vikosi vya Msaada wa Haraka vinavyoongozwa na Mohammed Hamdan Dagalo "Hemedti", naibu wa zamani wa Burhan katika Baraza la Utawala, vimeingia mwaka wake wa tatu sasa, na kusababisha vifo vya makumi ya maelfu ya raia.