Jarida la Al-Raya: Siri ya umuhimu wa eneo la mpaka wa pande tatu kati ya Misri, Sudan na Libya kwa wakati huu ni nini?!
Mji mkuu wa Misri, Cairo, uliandaa mkutano wa ngazi ya juu kati ya maafisa kutoka Misri, Libya na Sudan, ili kubadilishana mawazo juu ya changamoto na maendeleo ya kiusalama katika eneo hilo, kulingana na ripoti za vyombo vya habari, na ingawa hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusu mazungumzo hayo, chanzo cha habari cha Misri kililiambia " Mashariki ya Kati", kwamba lengo kuu la mkutano huo lilikuwa kujadili kuundwa kwa utaratibu wa pamoja kati ya nchi hizo tatu, kudhibiti usalama katika eneo la mpaka wa pande tatu, na kudumisha utulivu wa hali hiyo.