Machapisho ya Hivi Karibuni

Makala Iliyoangaziwa

null

null

Soma zaidi
Mfumo wa Jordan Unacheza Juu ya Fuvu za Watu wa Gaza kwa Kufadhili Tamasha la Jerash!

Mfumo wa Jordan Unacheza Juu ya Fuvu za Watu wa Gaza kwa Kufadhili Tamasha la Jerash!

Tovuti ya Al Mamlaka ilichapisha siku ya Jumanne, Julai 22, 2025, matamshi ya Waziri Mkuu wa Jordan, Jaafar Hassan, wakati wa kikao cha Baraza la Mawaziri katika Mkoa wa Jerash kuhusu ufunguzi wa Tamasha la Jerash, ambapo alisema: Tamasha la Jerash ni muhimu kwa uchumi wa mkoa na sekta ya utalii nchini Jordan, ambayo serikali inafanya kazi kwa uwezo wake wote na njia zake kuunga mkono na kukuza licha ya mazingira ya kikanda yanayoizunguka, na akaongeza: Shughuli za Tamasha la Jerash zitaanza Jumatano, akitumaini kuwa tamasha la mwaka huu litakuwa la kipekee zaidi na uwepo kuliko miaka yote iliyopita, kwani ni moja ya matamasha maarufu ya Kiarabu.

Ubinadamu unakataa kufurahia wakati watu wetu wanakufa kwa njaa!

Ubinadamu unakataa kufurahia wakati watu wetu wanakufa kwa njaa!

Katika zama za ujahiliya, ambapo nuru ya utume ilikuwa haijaenea, mtu mmoja kutoka kabila la Kikureshi alisema maneno ambayo ubinadamu uliyaweka milele, kabla ya utume kuyatakasa: "Ubinadamu unakataa kufurahia wakati watu wetu wanakufa kwa njaa." Alisema hivyo alipowaona Bani Hashim, wanaume, wanawake na watoto, wakisononeka kwa njaa katika bonde la Bani Talib, wakiwa wamezingirwa bila chakula wala kinywaji, huku yeye na watu wa Makka wakifurahia ufanisi. Mtu huyu na wenzake hawakungoja idhini kutoka kwa mtu yeyote, lakini hisia zao ziliamka, wakachana karatasi ya dhuluma, wakavunja mzingiro, na kusimama na aliyedhulumiwa, bila kusukumwa na itikadi, bali kwa msukumo wa kibinadamu.

193 / 10603