Enyi Waislamu: Elekezeni macho yenu kwenye majumba ya watawala wenu; na si Ikulu ya White House!
Macho ya Waislamu kwa ujumla, na waandishi wa habari, wachambuzi, waangalizi na wanaohusika nao haswa, yanaelekezwa kwenye Ikulu ya White House, na nini kitatokea katika mikutano ya Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa taasisi ya Kiyahudi Benjamin Netanyahu, na je! Trump atamshinikiza Netanyahu kuacha vita vyake dhidi ya Gaza?