Jarida la Al-Raya: Makubaliano ya Abrahamu Ni Uwezeshaji kwa Taasisi ya Kiyahudi au Laana Inayoashiria Kuangamia Kwake?!
Ni makosa kwa yeyote anayefikiria kuwa ukoloni ni enzi ya kihistoria tu ambayo imepita, kwani ukoloni ambao unafafanuliwa kama (kulazimisha udhibiti wa kisiasa, kijeshi, kiutamaduni na kiuchumi, juu ya watu waliokandamizwa kwa ajili ya kuwanyonya), kwa ufafanuzi huu, ukoloni ni njia ya kubeba kanuni ya kibepari ulimwenguni, kwa hivyo unabaki maadamu kanuni hii inaendelea kutawala ulimwengu na katika mahusiano ya kimataifa, kwa hivyo Magharibi kafiri mkoloni ndiye aliyeunda Mashariki ya Kati baada ya kubomolewa kwa Ukhalifa, na bado anaendelea kuishikilia na kuunda upya kwa njia ambayo inahakikisha masilahi yake.