Rada: Je, Makubaliano ya Abrahamu ni Nguvu kwa Taasisi ya Kiyahudi au Laana Inayoashiria Kupotea Kwake?!
Ni makosa kwa mtu kufikiria kwamba ukoloni ni enzi ya kihistoria tu ambayo imepita, kwani ukoloni, ambao unafafanuliwa kama (kulazimisha udhibiti wa kisiasa, kijeshi, kiutamaduni na kiuchumi juu ya watu walioshindwa kuwanyonyesha), kwa ufafanuzi huu, ukoloni ni njia ya kubeba kanuni ya kibepari kwa ulimwengu, kwa hivyo inabaki maadamu kanuni hii inaendelea kudhibiti ulimwengu na katika mahusiano ya kimataifa, kwa hivyo Magharibi kafiri mkoloni ndiye aliyeunda Mashariki ya Kati baada ya kuangushwa kwa Ukhalifa, na bado anaendelea kuishikilia na kuunda upya kwa njia ambayo inahakikisha maslahi yake.