Janga la Gabes, Mhanga wa Chaguo za Dola ya Kisasa ﴿NA ANAPOGEUZA MGONGO, HUFANYA BIDII KATIKA NCHI ILI AHALIFU HUKO, NA KUANGAMIZA MAZAO NA WATU, NA ALLAH HAPENDI UHALIFU﴾
Maandamano ya watu wa Gabes kusini mwa Tunisia yanaendelea kutokana na sumu zinazotoka kwenye kiwanda cha kemikali, ambacho kimegeuza jiji hilo kuwa eneo lililoathirika kimazingira na kiafya, na kuathiri moja kwa moja afya ya wakazi wa Gabes na maliasili zake, hivyo saratani na magonjwa ya kupumua yameenea, na mambo yamefikia hatua ya kukosa hewa mara kwa mara miongoni mwa wanafunzi. Miongo kadhaa ya ahadi za uongo na kupuuzwa kwa makusudi kumefanya Gabes kuwa ishara ya ubaguzi na uchafuzi, ambapo utajiri wa phosphate umegeuka kutoka baraka kuwa laana kutokana na sera za dola ya kisasa ambayo ilichagua faida ya haraka na maslahi ya makampuni makubwa kwa gharama ya afya ya watu na haki yao ya kuishi maisha ya heshima.