Hizb ut-Tahrir na Mradi wa Khilafa Rashidah: Mbadala Kamili wa Kistaarabu
Katika mazingira ya migogoro inayoendelea kuikumba dunia, na kufichuliwa kwa kushindwa kwa mifumo ya kisekula kushughulikia matatizo ya binadamu kwa njia ya kweli, kulizuka haja kubwa ya mradi wa kistaarabu wa kina ambao unamrejesha binadamu katika usawa wake, na umma wa Kiislamu katika nafasi yake, na kuwasilisha kwa ulimwengu mfumo uliokomaa katika utawala, huduma na haki. Katika muktadha huu, Hizb ut-Tahrir inatoa mradi kamili wa kisiasa unaowakilishwa katika kuanzishwa kwa Khilafa Rashidah kwa misingi ya Utume, kama dola ambayo inatekeleza Uislamu kwa njia kamili, na kubeba ujumbe wake kwa ulimwengu.